Wema Sepetu Adai Mwaka 2006 Ulikuwa Mwisho wa Miss Tanzania

Staa wa bongo movie,  Wema Sepetu ambaye pia aliwahi kuwa Miss Tanzania 2006 amesema hajui lolote kuhusu mashindano hayo zaidi ya kuwa mwaka alioshinda yeye ndiyo ulikuwa wa mwisho kwa mashindano hayo.

Hawa ndiyo walikuwa washindi watatu wa Miss Tanzania 2006,kulia ni Lisa (Mshindi wa 2),Kati ni Wema Sepetu (Mshindi wa 1) na Jokate (Mshindi wa 3).
Hawa ndiyo walikuwa washindi watatu wa Miss Tanzania 2006,kulia ni Lisa (Mshindi wa 2),Kati ni Wema Sepetu (Mshindi wa 1) na Jokate (Mshindi wa 3).
Mwaka jana mashindano ya Miss Tanzania yalifungiwa na BASATA kutokana na tuhuma za upangaji wa matokeo uliosababisha kupoteza msisimko na mvuto wa mashindano hayo. Hata hivyo mashindano hayo yamerejea tena.

Akiongea na Times FM, Wema alisema, “Sijui ni nini hasa kimetokea, maana mimi sifuatilii kabisa Miss Tanzania kwa sasa wala sijui Miss Tanzania mwaka huu anaitwa nani, nimeamua kuachana nayo kabisa sijui lolote, ila ninachojua mimi 2006 ndio mwaka wa mwisho wa Miss Tanzania.”

Bongo5

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mwaka 2006 ndo alitoka miss ushuzi mpaka leo hajatoka tena miss ushuzi kama yeye

    ReplyDelete
  2. Ninacho kumbuka mwaka huo 2006 ni kama ulishinda kwa figisufigisu wengi walitegemea Jokate angeshinda.....

    ReplyDelete
  3. wa tz kwa unafiki kama alishinda mwingine ilikuwaje atangazwe wema?

    ReplyDelete
  4. ulistahili kushinda una nyota nzuri, mbona hao wengine wa pili na watatu hatuwaoni wakinoga kivile???

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad