Rais wa TFF amesema bado wanasubiri taarifa kutoka CAF juu ya vurugu zilizotokea nje ya uwanja muda mchache kabla ya mchezo huo kufanyika huku akisema Yanga wasubiri kudra za Mwenyezi Mungu ili kuepuka adhabu kutoka shirikisho hilo la soka Afrika.
Hata hivyo Malinzi amesema Yanga bado ina nafasi ya kufuzu nusu fainali ya michuano hiyo kutokana na namna kundi lao lilivyo hadi sasa hivyo wao kama shirikisho wanawatakia kila la kheri katika maandalizi yao.
TFF mmekuwa wadhaifu sana juu ya swala hili tangu mwanzo,na hapo kuna jambo nyuma yapazia unalijua,tiririka Mkuu.Yanga inawakilisha TANZANIA hivyo ikienda kinyume ni aibu kwa TTF pia.
ReplyDeletemdau ngoja tuone hii sinema itaishaje,TFF hawako makini.
DeleteHakuna kusubiri kudra za mwenyezi Mungu kutoka CAF,na kama itakuwepo basi kuna mkono wa TFF.Adhabu itakayowakabili yanga ni ya TFF sanasana kwa uharibifu wa uwanja,na sio CAF.Kwani kwa hizo vurugu nje ya uwanja kuna mchezaji,au mgeni yeyote wa TP Mazembe au kiongozi yeyote aliyetumwa na CAF kaumia au kujeruhiwa?Na haka ingekuwepo,ni nje ya uwanja Yanga wasingewajibika chochote hapo.
ReplyDeleteJe kuna upotevu wowote wa mali zao?Kwa jinsi mlivyoongea na wanahabari ni kama hamjui chochote kilichotokea na kwamba ni uamuzi wa Yanga tu,hapo msikwepe TFF mmeshiriki kwa namna nyingine kwa hayo yaliyotokea,kwamba kama mngekuwa makini hayo yote yasingetokea.Kuna barua yoyote mliyoandika kwa Yanga kuwakataza kufanya au kuwapa mwongozo na hayo mliyoongea?TFF ni SIMBA & YANGA hapo ndio inakuwa shida,ni kukomoana tu,kamwe hatutasonga mbele ki-soka.
Na mna hasira za kukosa mapato,mweeh!
ReplyDelete