YANGA Yaambulia Kichapo Kitakatifu Kutoka Kwa TP Mazembe

June 28 2016 klabu ya Dar es Salaam Young Africans ilirejea katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam ambao ndio uwanja inaoutumia kama uwanja wake wa nyumbani kucheza mechi yake ya pili hatua ya nane bora dhidi ya klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo.

Katika mchezo huo wa Kundi A lenye timu za Medeama ya Ghana, Mo Bejaia ya Algeria, TP Mazembe ya Kongo na Yanga, umemalizika kwa Yanga kupoteza kwa goli 1-0, goli ambalo limefungwa dakika ya 74 Merveille Bope, TP Mazembe walionekana kucheza kwa umakini na uzoefu mkubwa, kitu ambacho kimeisaidia kupata point tatu.

Kwa matokeo hayo Yanga anakuwa kapoteza mchezo wa pili mfululizo, baada ya mchezo wa kwanza kufungwa kwa goli 1-0 na MO Bejaia ya Algeria, kwa sasa msimamo wa Kundi A unaendelea kuongozwa na TP Mazembe wenye point sita wakifuatiwa na MO Bejaia wenye point tatu, lakini wamezidiwa mchezo na TP Mazembe na Yanga.
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ndala poleni sana ndiyo ukubwa na muwe mnaukumbuka ule msemo usemao"MKAMIA MAJI HAYANYWI"

    ReplyDelete
    Replies
    1. Chura sports club jiandaeni kushuka daraja msimu ujao,
      bingwa atakuwa Mtibwa,mtake msitake.

      Delete
  2. Yenyewe TP mazembe iko juu sana afrika
    yanga wanakuwa muzuri,wameshangaza sana
    hapa kongo tumewakubali

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad