Zitto Kabwe Afunguka Tena ''CCM Wamdhibiti Magufuli, na Wasipomdhibiti Sisi na Watanzania Tutamdhibiti"

Baada ya taarifa za kutoweka, Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameibuka leo na kusema yuko salama wa afya huku akilaani mbinu za Jeshi la Polisi kutaka kumkamata kwa siri bila kufuata utaratibu unaotakiwa.

Tangu Jumamosi usiku, vyombo mbalimbali vya habari viliripoti Zitto kutofahamika alikokuwa baada ya simu zake zote kutopatikana huku viongozi wa chama hicho wakihofia kukamatwa na polisi baada ya kubaini njia za uviziaji wa kumkamata nyumbani
kwake.

"Ilikuwa Jumamosi , walikuja nyumbani kwangu wakiwa na magari matatu ila hawakufanikiwa, siwezi kukamatwa kwa `terms' zao ila nitakuwa tayari kukamatwa kwa `terms' zetu na wala siyo kuviziana, kama nina makosa kwa nini wanivizie," amesema Zitto Kabwe na kuongeza;

''Watu wetu wa Usalama wa Chama walihakikisha kwamba sitakamatwa ili niweze leo kupata fursa kuzungumza na watanzania kupitia nyie wana habari

''Hatufahamu Watawala wanaogopa nini mpaka kuzuia mikutano ya wanasiasa

''Nasikia Jana Walimkamata Mwenyekiti Mbowe wa Chadema Huko Mwanza kisa eti kawasalimia wananchi, huu ni uvunjwaji na ukiukwaji mkubwa wa utawala wa kidemokrasia

''Tunalaani tabia za Kidikteta za Rais Magufuli .Magufuli ameanza na vyama vya siasa kuonyesha Udikteta wake, nawahakikishia akimalizana na Vyama vya siasa atahamia kwenu Wanahabari, Tumkatalie

''Ndio maana Magufuli Ziara yake ya Kwanza alifanya Rwanda, tumegundua kuwa alikwenda kujifunza namna ya Kudhibiti Demokrasia na Kuongoza Kidikteta

''Hauwezi kupambana na Ufisadi kama haumpi nguvu ya Kiutendaji wa CAG. Kwa hali Hii anayokwenda Magufuli ajiandae kuwa rais wa term moja kwa sababu watanzania hawataweza kuvumilia kutawaliwa, kuminywa na kuburuzwa .

''CCM wamdhibiti Magufuli, na wasipomdhibiti sisi na Watanzania Tutamdhibiti

''Hatutakaa Kimya hata kama atatufunga, akimfunga Zitto watazaliwa wakina Zitto wengine, na kwenye hili hatutakaa Kimya, tutasimama kidete mpaka nchi irudi kwenye misingi''

''IGP ameagizwa na Magufuli anikamate, lakini hawezi kunikamata bila kufuata utaratibu, hawawezi kunikamata kwa kunivizia, viongozi hatukamatwi kwa kuviziwa viziwa, tumewaonyesha kwamba Polisi wanaweza kutukamata kwa kufuata terms zetu na sio zao

''Karibuni kesho saa tisa kwenye Kongamano letu, Hatuwezi kuacha kufanya siasa, lazima tuendelee kufanya siasa, mmehudhuria mikutano yetu hamjaona hata sisimizi amekanyagwa

''Wanasema Bajeti imeongezeka kwa 32% ukweli ni kwamba Bajeti imeshuka kwa maana Dola imeporomoka''

Post a Comment

22 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nanukuu,''NDIO MAANA MAGUFULI ZIARA YAKE YA KWANZA ALIFANYA RWANDA,TUMEGUNDUA KUWA ALIKWENDA KUJIFUNZA NAMNA YA KUDHIBITI DEMOKRASIA NA KUONGOZA KIDIKTETA''Hapo tudadavulie kama kweli una data na sio kudhani,(hapa inamuhusu Kagame na Magufuli)vinginevyo narudi kulekule kwamba Zito hii (ngondo)vita unaitafuta mwenyewe,kwa nini Unatangaza kwa uma kitu ambacho huna uhakika na hakina ukweli?

    ReplyDelete
  2. Kuna vyama vingi sana vya upinzani Tanzania,lakini tukubali tukatae kuna vyama ambavyo viko kwa ajili ya kuleta maendeleo,na kuna vyama ambavyo vyenyewe ni kuleta fujo tu.MTALAANIWA na Watanzania,Mungu ibariki TZ.

    ReplyDelete
  3. TATIZO WEWE ZITO NI NDUMILAKUWILI.

    ReplyDelete
  4. nafikiri zitto ni mgonjwa na inavyoonekana ugonjwa umeeingia kwenye akili maana anavyoropoka daa!!!!!

    ReplyDelete
  5. kama watu wako wa chama walihakikisha hutakamtwa mbona walikuwa wakitapatapa hawajui uko wapi hadi wakasema litakalokupata jeshi la polisi watajibu wao wacha fujo zako hatutaki na hatukukubali kabisa tunataka amani wewe utiwe ndani na hicho chama chako mpuuzi mkubwa wewe au jiuzulu ukae kimya kwenu sisi hatukutambui

    ReplyDelete
  6. Who the hell is you??? Usiseme sisi watanzania no hayo ni yako na msubiri TV huko Ukonga na siyo Bunge Live, wenye msimu mmoja ni nyie mnaojiita wapinzani
    Tafuta lugha siyo SISI ni wewe na wenzako wa Ukawa,, ama kweli safari imeiva na huku kutapatapa ndio dalili za mwisho wenu

    ReplyDelete
  7. Huyu mtu kaishachanganyikiwa na hana hoja sasa anabaki kubwabwaja bwabwaja. Hiyo yote ni kutafuta kiki tu. Unamtafuta tafuta Rais wetu kwa lipi hasa. Hiyo ya kubana matumizi ya Serikali ni jambo ambalo tuliishalitarajia tokea mwanzo. Na yeye Rais aliishayazungumza na kuyasisitiza kila mara. Kwani kama ni kweli suala la kupambana na ufisadi linaanzia kwenye ofisi ya CAG mbona ufisadi umekuwepo miaka nenda miaka rudi???? Wewe Zitto na wapuuzi wenzio tuelezeni ni agenda gani mliyoificha AMBAYO INAWAFANYA MKAE HAPO NA KUTAHARUKI TAHARUKI. Mnakalia hapo na kutoa visingizio hivi na vile kumbe kuna yaliyojificha nyuma ya pazia. Semeni hasa ni vitu gani nyie Wapinzani uchwara mnavyovitaka na ni kwa maslahi ya nani. Kwa sababu sisi Watanzania hatuoni kama mnatuwakilisha sisi na kama ni kweli mna maslahi mapana ya Watanzania wa kawaida. Hivyo vi information vyako visivyokuwa na kichwa wala miguuu usituletee hapa. Kama ni suala la Dollar ku flactuate kila siku inyokwenda kwa Mungu Dollar huwa ina flactuate depending on supply and demand. Acha uzushi mjinga mkubwa wewe huna lolote. Wewe na Ubunge wako wote uliokuwa nao pamoja na kuhama kila Jimbo la Uchaguzi mbona bado Kigoma inaongoza kwa umasikini kupindukia kulinganisha na Mikoa mingine. Wewe kama Mbunge unayehamia kila Jimbo la Uchaguzi pale Kigoma na kufanikiwa kuchaguliwa je umeusaidia kivipi huo Mkoa wako kuondokana na umasikini wa kupindukia??? Nadhani kabla hujamrukia Rais Magufuli na Serikali yake na Kujiweka kimbelembele na kuyazungumzia masuala ya Kitaifa ambayo yako nje ya uwezo wako. Kwa anza na kuyazungumzia masuala ya Mkoa wako wa Kigoma na utueleze sisi Wananchi wa kawaida ni kitu gani ambacho kimekufanya ushindwe kuendeleza Mkoa wako ili uondokane na umasikini. Na pili utueleze ni kitu gani hasa umekifanya kama Kiongozi unayehama kutoka Jimbo moja hadi jingine kuundeleza Mkoa wako. Wananchi wa hayo Majimbo unayoyaongoza wamefaidika nini hasa na uongozi wako. Kimsingi wewe ndio unaongoza kiimla zaidi na hiyo tamaa yako ya uongozi haitakufikisha mbali.

    ReplyDelete
  8. Big up zito. Watakuelewa Tu. Sasa watu wamelewa sifa wanasubiri viwanda wakati hazalishi chochote. Hongereni wadau wenye chuki Na zito. Elewa kuwa nchi ikiharibika hata WW hutokuwa salama. Tukana wanasiasa kwa kujenga hoja siyo kukosoa hoja. Zito endelewa hata ccm wanakujua ww Ni jembe. Hawa cdm wasikusumbue kwanza uliwasaidia Sana kujenga Chama kisha wakakutimua. Leo uko pekee yako Chama kimesimama. Watu wnaumiza vichwa jinc ya kukuzobiti. WW Ni jembe kaka

    ReplyDelete
    Replies
    1. Bingo zito
      Tupo nawe

      Delete
    2. Ni jembe gani ambalo limeshindwa kuuongoza Mkoa wake wa Kigoma mpaka hautamaniki kwa kiwango cha umasikini uliopindukia. Kama ni Jembe kweli basi na aanze kule kwa Kigoma kwa kuuondoa ule umasikini wa watu wa pale. Analitia sana aibu Kabila la Waha.

      Delete
  9. Nyote hapo juu yoooote menyewe

    ReplyDelete
  10. Nyie Wanasiasa uchwara wa upinzani msijifanye kama ni watu tofauti saaaaanaaa na Watanzania wengine. Nyie ni watu wa kawaida sana kama watu wengine wowote wale na mko chini ya sheria. Msijifanye kama nyie ni watu so special. Hakuna kitu kama hicho. Sasa kama mlifikiria hii Serikali ya sasa itawalealea kama zile Serikali zilizopita basi mmeula wa chuya kwani hapa ni kazi tu. Msipozitii sheria za Nchi na Mkizivunja zile amri zinazotolewa na vyombo vya dola basi itakuwa imekula kwenu. Mtaswekwa ndani na viboko juu halafu mtabakia hapo na kulaumulaumu eti hii Serikali ni ya kidikteta wakati Madikteta ni nyie wenyewe na maupuuuzi yenu ya kujiona eti ni miungu watu.

    ReplyDelete
  11. Na wewe Zitto Kabwe uache kujiona kama ni Mungu mtu. Wewe ni mtu wa kawaida sanaaaa huna lolote lile. Na kama ni Elimu basi Elimu yako ni ya kawaida sanaaaa. Na hizo mbinu zako chafu za kujificha na kutoa visingizio eti hauonekani sijui umekamatwa ama sijui vipi ni mbinu za kizamaniiiii zimepitwa na wakati. Unatumia mbinu za kizamani ili mradi tu ukidhi matakwa yako ya kipuuuzi ya kujiona wewe ni wa maana sana na kwamba ukipotea watu watababaiiikaaa. Hakuna kitu kama hicho mpuuuzi wewe. Kwan ukifa hata leo ni sawa tu kama mnyama porini hakuna atakayejali. Sana sana unajichora tu. Watu tunabakia kukushangaaa na maupuuuzi yako. Kwa kweli wewe Zitto kwa sasa umebakia kama katuni wa siasa. Hakuna heshima yoyote kwako. Ile heshima uliyokuwa nayo ndiyo hiyooooo imeishapotea na mwendokasi. Utabakia hapo unahanyahanya kama mwanamke malaya vile.

    ReplyDelete
  12. Mfu uliyefufuka ( hii kutikana na hao vijana ulipanga nao mikakati kutueleza kwamba umepote) Hana wa wewe mwenyewe jua umejichuria na karibu utapotea kweli.. Mimi na vijana wenzako tunaelewa kwamba umechanganyikiwa!! tusichokielwea ni ule ukubwa wa uchanganyikiwa wako ( Naomba mtusaidie kwa hilo) kama ni kichwa tim tim au netiwoki inapotea na kurudi?? Wewe sisimizi usiejaa hata katika kidole uwafundishe watu ( Hamisi Abdallah na Msafiri Mtemelwa) kuanzisha uzushi.. Tunakuuliza wewe na tutawauliza hawa waanzishaji wa Uvumi wamefanya hivi kwa mshinikizo wa nani/ walikuwa na lengo gani na jee huu uzushi ungewasaidiaje kufikia hayo malengo yao ya upotoshaji???? Je wewe unavyojijua katika hali yako ya kiafya hivi sasa na unaweza kuropoka na kubwabwajika kumzushia Raisi wetu na Jeshi letu la Polisi kwamba wanakuvizia !! Wewe zitto wa kuviziwa ( Una umuhimu gani hasa? ) kumbuka tarehe tuliyokupa ufike na kama ulidhani kwamba baada ya kueneza uszushi wako huu kwa kuwayumia hao vijana ni kwamba labda utatusitisha sisi kukuona jua.. Umekosea na unazidi kuleta vigezo ambavyo tutakuletea matatizo kisheria... Na tunakuonya tena uelewe vizuri hili onyo.. la kumuingilia na kuleta tahadhari zisizokuwa na upeo au uelewa na kukosa Maadili na kumkanya na kuwaeleza wana chama chake kuwa Wamdhibiti.. Kweli wewe sisimizi zitto unadiriki kutoa kauli kama hii kwa kingozi tuliomchagua sisi.. Je unazungumzha hizi pumba wewe kama nani katika nchi hii yetu yenye Amani utukivu na Usalama...Tena narudia hili ONYO MWANXZO NA MWISHO..Kama unaota mchana Madaraka basi jua ujue ni kali hapo njee.. linaweza kukuchoma na ni bora upumzike kimvulinu labada huo uji wako kichwa unaweza kuburudika.... Fika tarehe tuliyokupa bila kukosa mwana upotofu ulie jaa uchu na Chuki ya Roho yako mwentewe na utafikiria kuwashirikisha waliokuwe na wasiokuwemo... Kumbuka hii ni awamu yetu ya Tano.. Maamuzi hatuchukui haraka ila baada ya kuangalia kwa kina na tukitoa uamuzi unakuwa ni sahihi... watu wameshakuchoka na kila sifa isiyostahili kuwa nayo mtu wewe ndiyo nyumbani kwake... Inaelekea na inadhihirisha Haja ndugu zako na Jamii yako wanajuta wewe kuwa miongoni mwao.. Lakini dunia itakufundisha na vijiwe ni vingi ambapo unaweza kufit kutikana na TABIA YAKO ILIVYO... HAPA NI KAZI TU CHINI YA BABA JPJM...

    ReplyDelete
  13. HEeee !! Mwasiasa uchwara kumbe yuko hai?? Boda boda tu ndiyo iliyo umia na kuharibika... Kwa hiyo Khamisi Abdallah na Msafiri Mtemelwa ilibidi watoe habari zingine katika vyombo kuwa Tahadhari ilikuwa sivyo na kutudokezea kicho kuwa na walipo mpata huyo Dogo!! Haya Hamisi tunangoja ufafanuzi wenu na baada ya siku tutahitaji kuzumgunza na nyie pamoja na Msafiri... Kiki ilikuwa inatisha mnazungumza na Umma ama siyo??

    ReplyDelete
  14. zito tupe ukweli baba tunakupenda! kumbe bajeti imeshuka..? zitto wewe ni mti wenye matunda. tunaomba Mungu akulinde ila naamini hawakuwezi hao vibaraka wewe ni noma zito.. Pasua yote,. tumechoshwa na viongozi mizigo wanafanya usanii wao na kuuza magazeti.

    ReplyDelete
  15. zuto hana lolote na hakuna mtu mwenye chuki na zito kitu tunachotaka ni amani nchini jamani kumvukeni kuna watu wazima watoto hivo hamuoni nchi zisizokuwa na amani watoto wanvohangaika kitu amani tunataka

    ReplyDelete
  16. anonymous 5.03 i think you should go back to school we not here to fight for sisis au we what we need is peace you understand peace so wake up from your sleep Zito wont be with you when the country is up side down i repeat PEACE

    ReplyDelete
  17. kwani akihoji bajeti kuna tatizo gani?ana haki kikatiba,mbona watanzania hamjiamini na raisi wenu?kweni huyo raisi ni mungu?acheni hizo kabisa,nyerere mwenyewe alikuwa hana udikteta huo.

    ReplyDelete
    Replies
    1. RUDI SHULE KAJIFUNZE KUANDIKA NA WALA SI KUROPOKA CHIZI WEWE

      Delete
    2. Mimi ni M-TZ pia,kwa nini zito anahoji bajeti nje ya bunge?HALAFU nini kitaendelea baada ya hapo?hawezi kuchangia chochote bora angebaki bungeni hata kama angeonekana msumbufu lakini sisi wananchi tungemuona ana jitihada kwamba ni mtetezi,lakini nje ya bunge unaongea kitu kinachojadiliwa bungeni sio sahihi,ni uchochezi.

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad