Zitto Kabwe Aitwa Polisi Kwa Mahojiano

Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe jana tarehe 7/6/2016  aliitwa Polisi  na Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalumu ya Dar es salaam  ACP Camilius Wambura.

Kwa mujibu wa Katibu Itikadi, Mawasiliano na Uenezi wa chama hicho  Ado Shaibu, amesema ACP Wambura amemuita Zitto Kabwe kuhojiwa ikiwa ni siku moja imepita tangu azindue operesheni Linda Demokrasia ambayo inatarajiwa kuzunguka nchi nzima kupinga ukandamizwaji wa Demokrasia nchini

Amesema licha ya Zitto kuitwa na Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalumu ya Dar es salaam  Wambura aliomba Zitto  asiende jana kwa kuwa ni karibu na masaa ya kufuturu na  kumtaka  aende leo  saa tatu asubuhi.

Kwa upande mwingine  Shaibu amesema  Chama cha ACT-Wazalendo kitawasiliana na wanasheria wao ili kupata tafsiri ya kimahakama ya uhalali wa jeshi la polisi kuzuia mikutano ya vyama vya siasa ambayo inatambuliwa na kulindwa na katiba.

Post a Comment

15 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. ZITO ANAPOTEZA KILE ALICHOKUWA NACHO WAKATI ANAANZA SIASA.
    TATIZO NINI ZITO?MAANA HATA HUKU KWETU KIGOMA UPOUPO TU,HUELEWEKI.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umeonaa weeh!hata yule mama Anna anavutia kwani ana point.

      Delete
    2. Mshamba wewe zito
      Kasema kweli haswa
      Magufuli aache udikteta

      Delete
  2. tulimuamini lakini imani inakufa kwa zito kwa hali anayoenda nayo sasa hafai ni bora hata akili za kichaa

    ReplyDelete
  3. ndio maana alitimuliwa chadema

    ReplyDelete
  4. ubinafsi unamponza

    ReplyDelete
  5. zito wacha fujo wewe hata useme nini hakuna atakae pireza wakati kusoma watu wakiona suravyako tuu tunapata kichef kichef tulia baba wache wenye vipaji vyao yaani tumechoka kabisa unachusha

    ReplyDelete
  6. nasoro huna akili hata moja

    ReplyDelete
  7. Zitto..Amani ya nchi yetu..Ni jukumu la kila Mtanzania..Uchu wako WA madaraka Na siasa uchwara zilizo kushinda usiwe sababu ya Kivuruga Amani kwa upeo WA akili zako finyu Na zilizo kosa uelewa au Kama Ni uchu WA huko tulipo kusimamisha Ni kwamna hata sisi wananchi tumeshacboka Na wewe Na hatukutaki...zitto malizia kutafuta jiko Na atlest uwe Na majukumu ya nyumba..Uhuni wako WA kijiweni.mludi kijiweni Na kuangalia ustaarabu mwingine...la sera uchwara ngoja kipindi cha uchaguzi Kama Itakuwa hai Na afya njema...spidi ya uwajibikaji inawasumbua..Hapa Ni kazi Tu

    ReplyDelete
  8. Kabwe..Kama umeshaanza kuipoteza Netiwoki kichwani si bora ukajiamgalie afya hapo Mirembe...Mwisho Ni kubaya dogo!!! Manaake sikuelewi

    ReplyDelete
  9. Dogo je umekosa Amani katika moyo wakona spill over unataka kuwashirikisha waliokuwemo Na wasiokuwemo...Dogo pumzika Na siasa ambazo zimekushinda Na huna imahiri Na uzowfu nazo Na uchwara wako...na hakikisha unajipimzisha..au unatala uwe maarufu kila aiku gajetini Na fesibuku...tumekuchoka Na utokomeeeleeee mbali mpotoshaji Na fikra za uchochezi Na upotoshaji...hapa Ni kazi tu

    ReplyDelete
  10. Mfungeni Jela miaka 5 huyo Zitto atuache tuendelee na amani na kutafuta maendeleo ya nchi yetu. Asiambukize ukichaa wake kwa wananchi na kusababisha vurugu

    ReplyDelete
  11. Mwakyembe kasema Bungeni kuwa Werevu huongea tu wakiwa na jambo la kusema ila wajinga huongea ili tu wasikike hat kwa upuuzi ati hao Form four's Sugu, Msigwa na wengineo ku-doubt wenye PhD basi kazi yao ni kupinga wasomi tu
    Huu ndio mwisho wa upinzani na huenda baadhi yao watanusa jela kwa ujinga wa kutaka kusikika wakati hawana point ya kuongea
    Muone huyo Zitto hivi hamuoni mwenyekiti na muasisi wa chama cha ACT yuko kimya??? kasoma hivyo huongea tu akiwa na pointi ya kuongea
    Taabu sana Bongo

    ReplyDelete
  12. mbona watoa mada mapovu yanawatoka na mnaongea pumba?zito kwenye hotuba yake hajaongea lolote baya kaeleza ukweli,nyie subirini yawakute nyie sababu huyo rais wenu siyo mzima,ana element ya udikteta kabisa na uzuri hachagui chama.

    ReplyDelete
    Replies
    1. HATA WEWE NI RAIS WAKO,KAMA SIO WEWE BASI BABAKO YAKITUKUTA YATAMKUTA NA BABAKO.FYUUUU

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad