Zitto Kabwe Amjibu Rais Magufuli Kuhusu Kauli yake ya Kuvitaka vyama vya Siasa Kuacha Kufanya Kampeni

Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe amefunguka na kujibu kauli ambayo ametoa Rais Magufuli kuvitaka vyama vya siasa kuacha kufanya siasa mpaka kipindi cha kampeni tena katika uchaguzi wa mwaka 2020.

Zitto Kabwe ametumia ukurasa wake wa facebook kujibu kauli hiyo kwa kuonyesha kusikitishwa huku na kusema kauli hiyo wao kama wazalendo wanaichukulia kama ni vita dhidi ya demokrasia.
"Tumepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa kauli ya Rais kwamba vyama vya siasa havipaswi kufanya siasa isipokuwa wakati wa Kampeni na kupitia bungeni. Tunaichukulia kauli ya Rais Kama tangazo la vita dhidi ya demokrasia na uhai wa vyama vingi nchini. Chama chetu kitaitisha vikao vya dharura kujadili hali ya nchi na namna ya kukabiliana na mashambulizi yanayoendelea dhidi ya demokrasia nchini mwetu". Aliandika Zitto Kabwe

Mbali na hilo Mbunge huyo aliwataka wanasiasa pamoja na vyama vya siasa kuungana pamoja sasa katika vita hii dhidi ya demokrasia na kuacha tofauti zao ili kuweza kufikia lengo hilo.

"Tunatoa wito kwa Vyama vyote vya siasa nchini kuunganisha nguvu katika kuhakikisha tunapigana vita hii pamoja. Huu ni wakati wa vyama vya siasa na wanasiasa kuacha tofauti zao na kupambana kulinda uhuru wa kufanya siasa wakati wowote kwa mujibu wa Sheria. Tunatoa wito Kwa wananchi wote na taasisi za kiraia kusimama imara Katika Kulinda demokrasia. Tunasisitiza kuwa ushahidi wa kisayansi unaonyesha kuwa huwezi kuua demokrasia bila kuua juhudi za maendeleo. Tusiruhusu mtu yeyote mwenye mamlaka kuua demokrasia nchini mwetu". Alisisitiza Zitto Kabwe

Post a Comment

12 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. naogopa kukamatwa

    ReplyDelete
  2. Acha wewe umepotez mwelekeo na ubor ulio jijengea unaanza kudidimia. Heb ban Zitto jielew ndug laa sivy utakuj kujuta 2020.

    ReplyDelete
    Replies
    1. hivi kwa nini huyo raisi hapendi kukosolewa???chukua tahadhari ndugu yangu siyo mpaka akuchukulie mkeo au mumeo ndio ushtuke,nakupa mfano tu.

      Delete
    2. yaani wewe anony 10.25 ni mjinga yaani anavyofanya huyo zitto ni kwa jili ya kumkosoa rais au anafanya ujinga tuu? hata wewe nafikiri ni kama hiyo zito maana hujielewi

      Delete
  3. Tanzania umekuwa hivi mbona kazi
    Siasa ya ujamaaaaaaaa oyeeeeeeedr
    Mabepari mlie

    ReplyDelete
  4. wacha maneno yasio kuwa na msingi mjinga wewe usipenda amani mbn hujielewi wewe niwakuwekwa ndani na yeyote mwenye kero kama lako bwana tunataka amani na umuache raisi Magufuli afanyw kazi yake

    ReplyDelete
  5. Ni kweli atutaki siasa matope mda huu fanyeni kazi mda wa siasa ushapita. Kwa sasa watanzania tunataka maendeleo na sio siasa.

    ReplyDelete
  6. Kosa la zito lipi
    Like teja bungeni kulalamika eti kavuliwa kofia eti anatakiwa na yule mbunge mwanamke wa ukawa
    Hili teja ana nini alikuwa boyfriend wangu zamani nikamkacha kwanza hata chini hanaaaaaaaa
    Kiduchu
    Hata Suna hajenda anunuka hajioshi akikojowa
    Kanzu na filimbi wapi
    Fyuuuuuuuu

    ReplyDelete
  7. Udaku Eeeh.. Nakuombeni msituletee huyu ..mnamfata huko fesibuku halafu mnatuletea hapa.. Mimi nimeshamtoa katika like halafu nikamdeliti.. Ajili hana mpango huyuuuu!!! Nakuombeni tukimtaka tutamfa huko fesibuku.. Huko Mirembe anapata netiwoki? manakee yeye mwenyewe netiwoki inagonga mnara.. Sasa mlicho tuletea kaandika nini Mnawelew??? Msituletee tafrani asubuhi asubuhi... Zitti alikuwa siku zile miaka ile lakin si sasa kwenda mbele.... Msituletee tena upuuzi wake.

    ReplyDelete
  8. Udaku Eeeh.. Nakuombeni msituletee huyu ( Mwasasa Uchwara) ..mnamfata huko fesibuku halafu mnatuletea hapa.. Mimi nimeshamtoa katika like halafu nikamdeliti.. Ajili hana mpango huyuuuu!!! Nakuombeni tukimtaka tutamfa huko fesibuku.. Huko Mirembe anapata netiwoki? manakee yeye mwenyewe netiwoki inagonga mnara.. Sasa mlicho tuletea kaandika nini Mnawelew??? Msituletee tafrani asubuhi asubuhi... Zitti alikuwa siku zile miaka ile lakin si sasa kwenda mbele.... Msituletee tena upuuzi wake.

    ReplyDelete
  9. Hivi huyu ana tatizo gani??? Kama siasa ni kazi yako lakini kila kitu kwa wakati wake
    Mara oh tunaishitaki serikali mara or demokrasia imebakwa mara ohh Tulia hivi mara ohh tutangaze vita dhidi ya kuuwawa kwa demokrasia
    Hawa ishu yao ni moja tu ni BUNGE LIVE kwani wanataka kuonekana na kufika nyumbani na kumuuliza mwenzao "ULINIONA" majinga haya ni bahati mbaya kwa Tanzania kuwa na watu wenye fikra au mawazo kama hawa Mungu linusuru taifa letu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kupe wewe... yaani umetuona sisi watz ni vilaza sana hatuelewi kuwa hofu yenu ccm ndiyo inafanya kila kitu mnabana!!! fanyeni fair kama UK tu, ili tujipime...

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad