ZITTO KABWE:Serikali ya Magufuli Haipo Tayari Kukosolewa na Wapinzani Inatengeneza Mazingira ya Kuwanyamazisha

ZITTO Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo ameonya utawala wa Rais John Magufuli kuacha tabia ya kutaka kuziba midomo wapinzani.

Amesema, Serikali ya Rais Magufuli haipo tayari kukosolewa na wapinzani na kwamba, inatengeneza mazingira ya kuwanyamazisha sambamba na kuminya demokrasia.

Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Mjini amesema hayo leo baada ya kutoka kuhojiwa na Kamanda wa Upelelezi Mkoa wa Kipolisi wa Temeke na Naibu Kamanda wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa saa tatu.

“Mambo kama haya yalikuwa yanaanza kusahaulika katika mfumo wetu wa kisiasa nchi, lakini nyie ni mashahidi mnaona jinsi demokrasia inavyominywa na kuingia kwenye mashaka makubwa. Ni muhimu wananchi wakasimama kidete ili kuitetea demokrasia,” amesema Zitto na kuongeza;

“Wanatia woga wa watu kuzungumza mawazo yao ya kisiasa jambo ambalo si haki kwa kuwa ni sehemu ya wajibu wetu wa kisiasa. Hofu inayojengwa na serikali juu ya wanasiasa wa vyama vya upinzani haina maana.

“Kama leo polisi wametumia zaidi ya masaa matatu, hayo masaa waliyoyapoteza wangefanya kazi ya kupambana na majambazi, wahalifu na madawa ya kulevya badala ya kupoteza nusu siku kwa kutuhoji maswali,” amesema Zitto.

Anasema kuwa, ratiba ya kuzunguka mikoani itasitishwa kutokana na tamko lililotolewa jana na jeshi hilo.

Jeshi hilo limelizuia mikutano ya kisiasa hadi litakapotoa taarifa na kwamba, wanasheria wa ACT-Wazalendo  wataenda mahakamani ili kupata tafsiri sahihi.

“Lakini kama mnavyofahamu, jana limetolewa tamko la kuzuia mikutano yote hadi tamko lingine litakapotoka, hivyo basi tulikuwa tunashauriana na wanasheria ili wapate tafsiri ya kisheria kutoka mahakama kutokana na kwamba siyo sahihi polisi kuzuia mikutano.

“Lazima tuende mahakamani sababu bila ya kupata tafsiri ya mahakama, hatuwezi kufanya mikutano na hatutaki nchi iingie kwenye fujo,” amesema.

Steven Mwakibolwa, Mwanasheria wa ACT amesema kuwa, Zitto alihojiwa juu ya hotuba aliyoitoa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Jumapili wiki iliyopita na kwamba, yuko nje kwa dhamana isiyo na malipo.

“Tusubiri Jumatano wiki ijayo ili tujue kama atapelekwa mahakamani au upelelezi utajiridhisha kuwa hana makosa.

“Aliulizwa maswali mengi ambayo yalihusiana na hotu yake aliyotoa, amelezea kwa kina alichokisema maswali yote alijibu.”

Mwakibolwa amesema kuwa, kwa sasa si vema kueleza maswali aliyoulizwa kwa kuwa si muda na wakati sahihi wa kuliongelea suala hilo sababu liko chini ya upelelezi.

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. huyu zito hafai hata kuishi katika nchi yetu,zito sisi tunataka amani mbn una vurugu utawala wa rais magufyli tumeridhika nao na tunafuraha wewe kama huwezi bora ustafu kwenye hicho chama chako cha watu watatu kwa kifupi tunataka amani ccm oyee......... tuwachie nchi yetu wewe nina qasi wasi wewe sio mtanzania rudi kwenu

    ReplyDelete
  2. Zitto, Ama kweli !! Wewe Dogo lini utakua kiakili???? Unadiriki kusema leo polisi wamepoteza saa 3. ambazo wangeweza kuzitumia kupapambana na majambazi na watu wa madawa ya kulevya.. Yaani wewe unajua nini cha maana wao kufanya ( Unalifundisha jeshi letu la polisi vipaumbele) Jwe wewe madhara yako wasipo kushughulikia sasa unayajua??? Kua na utafakari unataka kuipeleka nchi yetu wapi???? Kukosa elimu na Uzalendo na Tammaa ya madalaka na kuwa magazetini kila siku inakupa shida..Jirudi na angalia hatima yako ni NINI.. manake sisi hatutokuwacha na hatuko tayari kuona amani inataka kuyumbishwa na wewe Dogo usiye na uelewa na Elimu finyu na Fikra Potofu... Na ndugu wa Magazeti nawaombeni kwanza mumuangalie huyu Dogo na kujua nia na lengo lake ni nini halafu mtapata Jawabu kama mumpe AirTime au laa.

    ReplyDelete
  3. Kabwe Zitto... Mimi si Shahidi wako. NOT ON MY NAME....Hilo ni skendo yako mwenyewe na usidhani tutakuonea huruma... Tumeshakujua na kukuchoka.

    ReplyDelete
  4. Ama Kweli... Maajabu, Hiyo Demoklasi unayo iimba unaijua maana yake?? Mkosa Elimu na Uelewa na mleta Siasa Uchwara zilizo kushinda wewe.. Pumzika au Posho inaleta tatizo... Njoo kama unavigezo vizuri ni letee CV inawezekana nikakupa ajira katika ofisi yangu ya sekurity Mwna wane.. poa Mwaya!! Angalia ustalabu mwingine.. Siasa huna umahiri nazo na zimekupiga chenga.

    ReplyDelete
  5. si unaona hadi umechosha watu kweli wasio na haya wana mji wao wewe sio waku simama tena na kuongea utumbo bwana hatukutaki tumechoka na tafarani zako hivo utakuwa lini tuwachie amani tanzania yetu tumeridhika kabisa na raisi jpm ondoka bwana nenda nyumbani mbn ziko kazi nyingi tu au bora urudi shule yaani umechosha kabisa wewe ni mjuaji sana hata chadema wamekutema sasa hapo ulipo hao jamaa zako wamechoka ila wanakupa muda tuu

    ReplyDelete
  6. huna akili zito ulijua utavuruga kumbe umejivuruga mi naona bora urudi shule ukasome maana inaelekea nawewe ni kilaza KASI IBNAKUTESA SANA MLIZOEA EEEEEEEEEEEEEEEEEE PORE SANA

    ReplyDelete
  7. YANAYOKUKTA ULISTAHILI NA NISAIZI YAKO UNAJIMALIZA KABISA DOGO

    ReplyDelete
  8. KAMA UNA LA KUSEMA BORA UKALALE

    ReplyDelete
  9. Zito acha kumwaga sumu Tanzania.

    ReplyDelete
  10. Ndio mazishi ya vilaza hayo
    Hawajioni kumbe ndio wanatoweka hivyo
    demokrasia uchwara hawa,, hawana ishu kwani Demokrasia yao ni madai ya Bunge Live
    Mwingine huko anajiita Raisi bila Ofisi ama kweli Upinzani wamesambaratishwa vibaya sana na inaonekana wote wamechanganyikiwa
    Waoneeni huruma kidogo labda kwa kuwapa Bunge Live kwani ni wengi hawawezi kupata kazi kwenye vituo vya TV kwa kuwa ni vichache au haviaajiri Vilaza???

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad