Watu 46 wamepoteza maisha na wengine 73 kujeruhiwa kutokana na ajali tofauti za mabasi ya abiria na magari mengine katika kipindi cha wiki moja iliyopita hapa nchini.
Watu 46 wamepoteza maisha na wengine 73 kujeruhiwa kutokana na ajali tofauti za mabasi ya abiria na magari mengine katika kipindi cha wiki moja iliyopita hapa nchini.
Takwimu hizo zimetolewa na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, wakati akiongea na waandishi wa habari ambapo amedai baadhi ya ajali hizo zimesababishwa na uzembe wa madereva na mwendokasi.
Kamanda Mpinga amesema, madereva wamekuwa wakikiuka kwa makusudi sheria inayowataka kuendesha kwa mwendo usiozidi kilomita 80 kwa saa, baadhi ya abiria kushangilia mwendokasi bila kutoa taarifa kwa vyombo husika na kwa upande mwingine, baadhi ya wamiliki wa magari hayo kuwapa motisha madereva ambao wanavunja sheria, pale wanapowahi kufika vituo vya mwisho na kuwalipia faini pale wanapokosea