Aliyeongoza Jaribio la Mapinduzi Nchini Uturuki Akamatwa

Jenerali Erdal Ozturk (katikati) aliyekuwa kinara wa jaribio akiwa mikononi mwa wananchi.

Jenerali Erdal Ozturk aliyekuwa kinara wa jaribio lililoshindikana la mapinduzi ya rais nchini Uturuki amekamatwa, huku viongozi wengine wa mapinduzi hayo, saba wakifanikiwa kutoroka na kukimbilia nchi jirani ya Uturuki kwa kutumia Helikopta.


Jenerali Erdal Ozturk (kulia) enzi akiwa kazini.

Hata hivyo viongozi hao waliokimbilia nchini Uturuki wakiwemo mameja wawili, makapteni watano na raia mmoja wamekamatwa nchini humo kwa kile kilichoripotiwa kuingia nchini humo bila kibali.Jenerali Erdal Ozturk aliyekuwa kamanda mkuu wa kikosi namba tatu tayari amekamatwa na kuwekwa mahabusu wakati akisubiri hatma yake na huenda akanyongwa ikiwa atapatikana na hatia hiyo.

Mapinduzi hayo yalishindikana baada ya wananchi wengi kujitokeza kumsapoti Rais Recep Erdogan, ambaye ametamka bayana kwamba wote waliohusika na jaribio hilo lililoshindikana watakabiliwa na adhabu ya kifo.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Point of Correction: Nchi iliyotaka kupinduliwa ni Uturuki na waliotoroka wamekimbilia Uturuki!! [-(

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad