Baada ya Kuchuniana Muda Mrefu...Wema Sepetu Amtakia Happy Birthday Kajala

Miezi sita iliyopita, Wema Sepetu alikuwa na hasira na Kajala kiasi cha hata kuthubutu kusema hamjui.

“Mimi mtu ambaye sitaki kujiassociate naye namtoa kabisa ndio maana naweza nikakaa nikakuuliza Kajala ni nani? Huu sio muda wa kumzungumzia na kumpa airtime,” Wema alimuambia Zamaradi Mketema kwenye kipindi cha Take One cha Clouds TV kilichoruka January mwaka huu.

Na sasa huenda Wema ameanza kuufungua moyo wake na kutafuta sehemu ndogo ili kumsamehe. Leo ni siku ya kuzaliwa ya Kajala na Wema ameungana na mastaa wengine kumpongeza muigizaji huyo.

Wema ametumia post tatu kwenye Snapchat kumpongeza Kajala.

Wawili hao waliwahi kuwa marafiki wakubwa miaka miwili iliyopita ambapo Wema alimlipia Kajala shilingi milioni 13 ya hukumu aliyopewa mahakamani kwa kesi iliyokuwa ikiwakabili na aliyekuwa mume wake.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Anaona hata akimnunia mwenzie mambo yake yanazidi kunyooka ataacha kujishusha ila akumbuke akiwa na hasira ajizuie kuongea maneno mabaya kwani hasira zitaisha ila maneno ayatasaulika

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad