Baby Madaha akanusha kufunga ndoa, alivishwa pete ya uchumba

Msanii wa filamu na muziki, Baby Madaha amekanusha taarifa ambazo zilizagaa katika mitandao ya kijamii kuwa amefunga ndoa na mwarabu wa Dubai.


Mapema mwaka huu gazeti moja kubwa liliripoti taarifa ya kuwa msanii huyo wa filamu alifunga ndoa kimya kimya na mwarabu wa Dubai baada ya ukukubali kubadii dini na kuwa muislam.

Akiongea na Bongo5 Jumanne hii, Baby Madaha alisema kilichofanyika wakati huo ambacho kinadaiwa ilikuwa ni ndoa, ulikuwa ni utambulisho wa mpenzi wake huyo kwa wazazi wake.

“Ndoa bado sijafunga kama baadhi ya watu walivyosema ila nimeveshwa pete ya uchumba na nimemtambulisha mpenzi wangu kwa wazazi” alisema Baby Madaha.

“Kusema kweli kila kitu kinaenda sawa na tayari nimeshavalishwa pete ya uchumba, sema sikutaka kutangaza kwa sababu wasanii wengi wamekuwa wakiishia katika pete za uchumba, kwa hiyo niliona nikishafunga ndoa ndio nitaweka wazi,” aliongeza.

Pia mwigizaji huyo amesema amekubali kubadili dini na kufunga ndoa ya kiislam.

“Unajua sisi wasichana, watu wanasema hatuna dini, kwa hiyo mimi binafsi kama mama yangu akiwa tayari nitafunga ndoa ya kiislam kwa sababu haya ni maisha,” alisema Baby Madaha.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Sawa Sawa mwaya haya ni maisha kwanza dini zenyewe hazina tofauti kubwa zote zinamwamini mungu alieziumba mbingu na nchi. Na madili yale yale, amri zile zile, kikubwa upendo. Umempenda kakupenda dini ni Imani tu iliyojengeka kwa mtu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad