Balozi Sefue afunguka..Adai Wakati wake Umefika Sasa

Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu, Balozi Ombeni Sefue amesema baada ya miaka mingi ya utumishi wa umma sasa ni wakati wake wa kupumzika na hafikirii kujitosa katika siasa.

Balozi Sefue ambaye alikuwa kivutio kwenye televisheni kutokana na kutoa taarifa za kutenguliwa uteuzi kwa watumishi waandamizi wa umma kabla ya kibao kumgeukia, amesisitiza kuwa siasa haipo katika damu na kwamba kazi anayopenda ni kuzisaidia taasisi za ujenzi kwa kuwa ni taaluma anayoipenda.

Mbali na kuonyesha kutokuwa na mpango huo, Balozi Sefue aliupongeza utendaji kazi wa Serikali ya Awamu ya Tano kwa maelezo kuwa una kasi nzuri na kwamba kurejea kwa uadilifu ni jambo linalomfurahisha zaidi akiwataka vijana kufanya kazi kwa bidii baada ya kuaminiwa na kupewa nafasi mbalimbali.

Balozi Sefue ambaye awali hakuonekana kuwa mmoja wa watu ambao wangeng’olewa kwa sababu yoyote ile, alilazimika kuondoka Ikulu ndani ya siku 123 tangu Rais Magufuli aapishwe kuwa Rais na siku 67 tangu balozi huyo atangazwe kuendelea na wadhifa wake. Uteuzi wake ulitenguliwa Machi 6 na nafasi yake kuchukuliwa na Balozi John Kijazi.

Baada ya kimya cha muda mrefu, Mei mwaka huu, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais (Utumishi wa Utawala Bora), Dk Laurean Ndumbaro alikaririwa akisema kuwa baadhi makatibu wakuu walioachwa katika uteuzi na Rais, wapo waliostaafu kwa mujibu wa sheria, akiwamo Balozi Sefue.

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Balozi Sefue, Utendaji wako ulikuwa ni moja ya nguvu ambayo ilitupa kasi hii tunayo enda nayo sasa.. Tunakukumbuka kama ni mmoja wa watendaji waanzilishi wa mwelekeo wetu huu kwa ushirikiano ulitoa kwa Mh Rais JPJM. Pia maadili na Nidhamu uliyo kuwa siku zote unaiangalia katika utendaji wako ilikupa ufanisi mkubwa na Juhudi ulizofanya awali mara ya Mh Rais kuingia Madarakani ulikuwa ni mmoja wa nguzu katika utendaji hapa Ikulu. Na tunakuahidi kuwa sisi utumejifuzo mengi katika utendaji na ufanisi na hatuto sita kutaka ushauri wako pindi tukiuhitaji. Tunakushukuru kwa Uzalendo na Imani na uvumilivu wa kustahamili uliyotuonesha kwa muda wote ulipokuwa Madarakani, Tunakuombea Mungu akupe Afya njema na Umuri mrefu na mapumziko yaliyo salama. Sisi ni ndugu zako / Kaka zako / wadogo zako / Rafiki zako.. Tunakwambia tuko pamoja wakati wowote unakarishwa na ukihitajika hatutosita tutakufata na ushaurri tutachukua kwa nia na lengo la kuboresha na kurekebisha / kukushirikisha kwa manufaa ya nchi na wananchi.. HAPA KAZI TU...Chini ya Baba JPJM na wewe ukiwa ni mmoja wa waanzilishi wa timu yetu Kabambe.. Tunakushukuru kwa Uzalendo wako uliouonesha kwa wakati wote.

    ReplyDelete
  2. Balozi Sefue, Utendaji wako ulikuwa ni moja ya nguvu ambayo ilitupa kasi hii tunayo enda nayo sasa.. Tunakukumbuka kama ni mmoja wa watendaji waanzilishi wa mwelekeo wetu huu kwa ushirikiano ulitoa kwa Mh Rais JPJM. Pia maadili na Nidhamu uliyo kuwa siku zote unaiangalia katika utendaji wako ilikupa ufanisi mkubwa na Juhudi ulizofanya awali mara ya Mh Rais kuingia Madarakani ulikuwa ni mmoja wa nguzu katika utendaji hapa Ikulu. Na tunakuahidi kuwa sisi utumejifunza mengi katika utendaji na ufanisi wako na hatutosita kutaka ushauri wako pindi tukiuhitaji. Tunakushukuru kwa Uzalendo na Imani na Uvumilivu wa kustahamili uliyo tuonesha kwa muda wote ulipokuwa Madarakani, Tunakuombea Mungu akupe Afya njema na Umuri mrefu na mapumziko yaliyo Salama. Sisi ni ndugu zako / Kaka zako / wadogo zako / Rafiki zako.. Tunakwambia tuko pamoja wakati wowote unakaribishwa na ukihitajika hatutosita tutakufata na ushauri tutachukua kwa Nia na Lengo la kuboresha na kurekebisha / kukushirikisha kwa manufaa ya Nchi na Wananchi.. HAPA KAZI TU...Chini ya Baba JPJM na wewe ukiwa ni mmoja wa waanzilishi wa timu yetu Kabambe.. Tunakushukuru kwa Uzalendo wako uliouonesha kwa wakati wote.

    ReplyDelete
  3. Mungu akulinde siku zote

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad