CAF Yailima Klabu ya Yanga Faini ya Million 22

Klabu ya Yanga imepigwa faini ya dola za kimarekani 10,000 ambazo zinakadiriwa kufikia shilingi milioni 22 za Tanzania kwa kosa la wachezaji wake kuchelewesha muda ili mchezo usiendelee wakati mwamuzi alipotoa adhabu ya penati kwenye mchezo wao wa marudiano dhidi ya Sagrada Esparenca ya Angola.

Mtandao rasmi wa CAF umeripoti kwamba, Yanga imepewa fursa ya kulipa nusu ya kiasi hicho kwa maana ya dola 5,000 zinazokadiriwa kuwa sawa na shilingi milioni 11 za Tanzania na italipa kiasi kingine endapo itarudia kosa kama hilo.

CAF pia imeitoza faini ya dola 10,000 klabu ya MO Bejaia ya Morocco kwa kosa la mashabiki wake kurusha fataki kwenye mchezo wao wa kwanza hatua ya nane bora dhidi ya Yanga uliochezwa mjini Bejaia, Morocco.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. kumbe ngoma droo,walioendelea na walioishia pale wote wamepigwa faini!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad