KATIKA kutekeleza tamko la Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha) la kufika Dodoma kusaidiana na Jeshi la Polisi kuzuia Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bavicha Dodoma wameanza maandalizi ya kupokea vijana zaidi ya 2000.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana Malambaya Manyanya, Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa Dodoma alisema, kwa sasa viongozi wa mkoa wameanza maadalizi ya kuwapokea wageni wao ambao wanatarajiwa kuanza kuwasili tarehe 21 na 22 Julai mwaka huu.
Alisema, maadalizi hayo ni ya kuwapokea vijana ambao watatoka katika mikoa yote ya Tanzania kwa lengo la kutimiza tamko la Bavicha taifa la kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma kuzuia mikutano na vikao vya CCM.
Alisema, kwa sasa mkoa tayari umeunda kikosi cha kufanya kazi ya maadalizi ya ugeni huo ambapo kwa nia njema utafika mjini Dodoma kutekeleza kauli ya Rais John Magufuli ya kuzuia vikao vyote na mikutano ya vyama vya siasa.
Alisema, maadalizi hayo ya kuwapokea vijana hao ni pamoja na viongozi wa kitaifa wa Bavicha kwa maana ya kutafuta mahali pa kulala na maandalizi ya chakula.
“Wapo watu ambao wanadhani Bavicha wana mpango wa kufanya fujo, sisi tunataka kurejesha Demokrasia nchini na kutekeleza kauli ya mkuu wa nchi.
“Tumekuwa tukiona jinsi mikutano ya Chadema inavyozuiliwa, na sasa msimamo wa Bavicha ni kuzuia mkutano ya CCM unaotarajiwa kufanyika Julai 23 kwa lengo la kubadilishana uongozi kati ya mwenyekiti wa sasa wa CCM na rais msitaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete na Rais John Magufuli.
“Tumeandaa vijana takribani 2000 kutoka mikoa yote nchini watakaokuja Dodoma kusaidiana na Jeshi la Polisi kutawanya mkutano usio halali wa CCM.
“Kwa sababau mkuu wa nchi ametoa tamko la kuzuia mikutano yote ya siasa ikiwa ni pamoja na vikao vya ndani na mikutano ya hadhara hadi 2020.” Alisema Malambaya.
Alisema, Jeshi la Polisi lilizuia mikutano ya vyama vya siasa vya upinzani na mahafali ya Jumuiya ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Chadema (CHASO) na kuwa, sasa wanashirikiana na polisi kuhakikisha mikutano ya CCM haitafanyika.
poleni sana maana kipigo mtakachokipata hamtarudia tena
ReplyDeletevijana wenzangu nawaasa acheni kwenda huko mtaumia
ReplyDeletekila mtanzania kwa imani yake aiombee nchi yetu
ReplyDeleteRais Magufuli ndiye anayasababisha haya. Kauli zake ambazo hazipimwi zitatuletea madhara. Tz ni yetu sote. CHADEMA wana HAKI SAWA na CCM. Aiondoe hiyo kauli yake.
ReplyDeleteWewe uko salama hapo kwenye nywele???? au zimeja nyewele tu!!!
DeleteHivyo mlipewa mwaliko wa kuta usaidizi wenu kutoka Jeshi letu la Polisi? na malazi itakuwa kambi ipi mliyopangiwa kabla ya utekeleza wa hayo maombi ili mpangiwe majukumu??? Wahenga walinena MWIBA YA KIJITAKIA UKIKUCHOMA..... Mungu alikupeni akili ila inaelekea utumiaji wenu si sahihi na Kwa Taarifa yenu ... MIREMBE IMEBAHATIKA KUWA HAPO HAPO DODOMA.. karibuni kabla ya Kupangiwa majukumu ili tuweze kuwasaidia Kiafya...Tatizo mnalo na kuwashughulikia kwetu si tatizo ila ni wajibu wetu. Karibuni sana Vijana sema mtuone kabla ya kuanza utekelezaji na barua ya mwaliko mje nayo!!!!!!!!!!!! fyuuuuu.... Hapa Kazi tu

Delete