CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimepanga kulisaidia Jeshi la Polisi kuzuia Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Hivi karibuni Jeshi la Polisi lilitoa zuio la mikutano ya siasa ya wazi na ya ndani nchini kote, hata hivyo CCM imepanga kufanya Mkutano Mkuu tarehe 23 Julai mwaka huu mjini Dodoma.
Kwenye mkutano huo, Dk. Jakaya Kikwete, Mwenyekiti wa CCM atakabidhi mamlaka hayo kwa Dk. John Magufuli ikiwa ni utaratibu wa kawaida wa chama hicho.
Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha) limepanga kuzuia mkutano huo kwa madai ya kulisaidia Jeshi la Polisi kusimamia agizo lake kwa vyama vya siasa nchini.
Wakizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Slaam viongozi wa Bavicha walisema, hatua hiyo ni katika kuhakikisha wanalisaidia jeshi kutekeleza amri iliyotolewa na Rais Magufuli ya kuzuia mikutano ya vyama vya siasa hadi mwaka 2020.
“Tumeandaa vijana takribani 2000 kutoka mikoa yote nchini watakaokwenda Dodoma kusaidiana na Jeshi la Polisi kutawanya mkutano usio halali wa CCM. Kwa sababau Jeshi la Polisi limezuia mikutano yote ya siasa kwa sasa.
“Pia ni katika kuunga mkono kauli ya Rais Magufuli kwamba, hakuna mikutano ya vyama vya siasa mpaka mwaka 2020. Huu ndio msiamamo wa baraza.
“Mikutano yetu sisi kama Chadema tunazuiwa lakini CCM wanafanya. Mahafari ya chama cha mapinduzi yanafanyika. Ni jana CHASO (Jumuiya ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Chadema) Morogoro tumezuiwa lakini UVCCM (Umoja wa Vijana wa CCM) Mkoa wa Morogogo wamefanya na picha zipo. Hii sio haki, kama mbwai na iwe mbwai,” alisema Patrick ole Sosopi, Makamu Mwenyekiti wa baraza hilo.
George Tito, Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa Mbeya alisema “… ni kwamba, huko mikoani vijana wameshajipanga. Wana ari kubwa ya kwenda Dodoma.
“Tumeamua kufikia hatua hii kwa sababu tumekuwa tunaona hakuna haki katika nchi hii. Kuna mahafali yanafanyika vyuo vikuu, wenzetu CCM wanaruhusiwa sisi Chadema tunakatazwa.Vijana wa Chadema wamekuwa wakikamatwa bila sababu za msingi,” alisema Tito.
Na nyie vijana mlioandaliwa ni wajinga sana maana mtaishia kuumizwa Na vyombo vya dola Na baadaye kunyea debe magerezani. Huo siyo mkutano wa siasa ni Kukabidhi madaraka na siyo jambo geni ila nyie chadema mnataka vurugu tu. Cheza na aliyeshika mpini uone cha moto. .......
ReplyDeleteTanzanians are cowards of the first order. The country will never move forward with this mentality of one man show. Parties should practice their constitutional right freely. The comment of Makoye is very unfortunate statement and of semi illiterate. The nation doesn't belong neither to CCM nor Magufuli. It is bigger and important than any of the two.
ReplyDeleteWhoever you are. Please refrain from using such words. The way you look forward is hazy. I'm not sure if you is a human a giggy machine response who is no
DeleteTito / Mbwae na wote wenzenu.. Kumbuka jeshi la Polisi halijaomba Msaada wenu.. Nyinyi mnahitaji kusaidiwa baada ya Dhana Ovu wa kuwatosa wenzenu ambao hawajielewi...Au mliletewa mwaliko wa kuomba msaada wenu na mletaji alikuwa ni Nani na lini mmmelezwa kuwa muwe mmesharipoti Vituoni ili mpangiwe majukumu?
ReplyDeleteNashauri wazazi wawasihi watoto wao. Wanaanza kuvuka mipaka kisa Siasa. Wanakoelekea sio. Acha kabisa kucheza na dola wataumia na Historia itaandikwa Tanzania kwamba kulikuwa na Vijana fulani kilichowakuta...... ..........................Kila lakheri Bavicha.
ReplyDeleteFikirini kabla ya kutenda wajinga nyie,hapo hutaona mtoto wa kiongozi wenu hata mmoja.
ReplyDeleteNILIWAHI KUSOMA HAPA MDAU KAANDIKA KWAMBA YEYE YUKO RADHI KULA MLO MMOJA KWA SIKU KULIKO KUKOSA AMANI NCHINI,AMA HAKIKA ALIONA MBALI.MNACHOTAKA KUKIFANYA NI KUVUNJA SHERIA NA KUCHOCHOA VURUGU.HATA MIMI NAMUUNGA MKONO,JAPO KUWA NAWAPENDA CHADEMA LAKINI KWA HILI HAPANA.JAMANI KAMA MNA HAMU YA KUSAIDIA POLISI OMBENI KIBALI KWAO INGIENI MITAANI MKISAIDIANA NA SUNGUSUNGU KUDHIBITI WAHALIFU/VIBAKA.TUTAWAPENDA KULIKO UJINGA HUU MNAOWAZIA KUUFANYA.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
ReplyDeleteWee uliyeandika comment zako tunajua siyo mtanzania na ndiyo maana unataka kuweka mbele demokrasi za kijinga. Huwezi kumwambia mwnzako ni semi-illetrate, wewe kujua kiingerza unaona ni hoja ya msingi, mbona hata mashoga wanajua lugha hiyo hata kukushinda wewe? acha kutawaliwa kimawazo maana una tofauti na mfu. Uhuru gani unaoutaka? kutofanya kazi na kushinda mjini kunyatia wazungu? au maandamano yasiyo na tija? acha ujinga wakati babako na mamako hawana hata senti nyeupe wewe unaona kiingereza nimtaji. Issue hapa hao UKAWA waliozuia mikutano yao ni ccm au polisi? wao kama ni haki basi wazuie mikutano ya polisi na mbona walishindwa majuzi viwanja vya BIAFRA? hakuna platform ya hoja husika. Ni Mtazamo wangu.
ReplyDelete