Chadema watangaza mikutano ya hadhara Na Maandamano Nchi Nzima kuanzia Septemba Mosi....

Kufuatia kile walichokiita 'matukio ya ukandamizaji wa haki na demokrasia',   Chadema kimetangaza Septemba Mosi mwaka huu kuwa siku ya mikutano ya hadhara nchi nzima.

Chama hicho pia kimezindua Operesheni Ukuta (Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania),  huku kikiwataka wananchi wote waliokumbana na 'rungu'  la Serikali ya Awamu ya Tano kuungana na Operesheni hiyo,  wakiwemo mama ntilie na waendesha bodaboda.

Chama hicho kimetaja mambo 11 kinachodai kuwa yamefanywa na Serikali bila kufuata sheria na kanuni za nchi,  likiwemo la kuzuiwa kwa shughuli za kisiasa na kutaja sababu 24 za kuibuka na Operesheni Ukuta

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. haya mwenyekiti
    kazi imefika patamu
    pambaneni tuone nani anaweza na siyo kutumia POLISI KISA AMANI NA UTULIVU NIMELISIKIA HILI NENO TANGU NIKIWA MTOTO ENZI YA MKAPA NIMECHOKA NA HILI NENO
    Watanzania tunajua PUMBA NA MCHELE
    PEOPLES POWERRRRRRRRRR

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wee kama umechoka kusikia neno amani na utulivu nenda somalia,au hata burundi acha sisi tunaolitaka hilo neno tuendelee kulisikiliza.

      Delete
  2. Mfyuuuuuh! Nilijua hawana jipya, ni yale yale isipikuwa wameyatafutia attention.....hovyoooo, katika hayo maandamano muhakikishe na wake zenu na familia zenu wanashiriki, msiwaponze wengine wakavunjwa miguu, nyinyi viongozi na familia zenu mnatunga safari......UJINGA NI WAKATI WA KWENDA, HATUDANGANYIKI............

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni wewe mjinga.nenda shule pata elimu.wewe nikilaza mmoja mkuu wa Tanzania. Sijui kama umesoma au unababaisha mitaani tu.nani avunje miguu. Ndo udictator tunaousemea. Polisi wamesema hawajazuia mikutano ya hadhara. Wameacha CCM kufanya mkutano na mwra zote kukanusha hadharani hamuna aliyezuia. Elimu.

      Delete
    2. yaani katika wajinga wewe anony 6.42pm ni mjinga sana nani dictator kama si mwendwawazimu mwenziyo mbowe aliyeng'ang'ania uwenyekiti kwa miongo mingi???? CCM haikufanya mikutano ya nje kama nyinyi mlivyokuwa mnafanya, acha uzembe wa akili mjinga wewe. tena wewe ndo unatakiwa uende shule kwa sababu ukilaza wako umevuka mpaka, acha ujinga pumbavu zako

      Delete
  3. Hayo maandamano na mikutano ianzie Moshi na Arusha, msitake kuwapotezea watu wa kanda nyingine muda wa kufanya shughuli zao, huko kwenu watulie wakiendelea na kazi na biashara zao, HAPANA! Hiyo ajenda yenu ya siri TUMEISTUKIA......HAPA KAZI TU!

    ReplyDelete
  4. Kufanya mikutano na maandamano ni haki ya kila mtanzania.

    ReplyDelete
  5. Hao viongozi ndio wanaopaswa kuwa mstari wa mbele kuandamana, na sio kuwatanguliza bodaboda na kina mama wasiojua lolote kuhusu siasa uchwala. Mimi kama MPINZANI haya mambo yaliisha pita baada ya uchaguzi, Sisi kama wapinzani tunatakiwa kujipanga upya kwa ajili uchaguzi ujao 2020. Mimi mwenyewe siipendi ccm siwezi nikamchukia MTanzania mwenzangu kisa yeye ni Ccm. Ndugu zangu wa upinzani huko tunakoelekea sio kuzuri, inaonekana vurugu tupu, hata kama wanachama wanarudi ccm basi upinzani kuna kasoro

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad