Mrembo na Mtangazaji wa Clouds FM amemuomba Paul Makonda Kuwatumbua Wamiliki wa Nyumba za Kupanga Dar es Salaam kwa Kufanya Haya:
Soma Alichoandika Kupitia Ukurasa wake wa Instagram:
"Jaman naomba mu m tag Mheshimiwa Makonda Mwambieni Nyumba tunalipishwa kwa Dola na tunalipa miezi 6 hadi Mwaka wakati mshahara tunalipwa Kila Mwezi na Tunakatwa Kodi inaenda serikali yaan kwa ufupi kuna makato sana , Mwambieni yaan sisi independent tunaumia sana mahela ya nyumba mengi sana watuonee huruma , Kwann tusiwe tu kama nchi nyingine tulipe mwezi mwezi na hamna kulipa dalali. Maana asilimia 90 ya wakazi wa Dar es salaam wanalalama na suala la nyumba ermmm atusaidie kwenye hili Tatizo. Dalali anachukua kodi ya mwezi Mzima bila huruma or else hupewi nyumba hilo timbwili lake , na walipe kodi na wao pia , huo msako wa Nyumba kwa nyumba uhusishe pia kuangalia is it worth na kodi mtu anayolipa maana yaan ts hectic , mwambieni kama kweli anatujali wakazi wa Dar es salaam na yeye ni Mkuu wa Mkoa wetu atoe tamko. hamna kulipa Madalali, Na nyumba kodi mwezi mwezi kutokana na system ya ulipaji wa mshahara Pia. maana hatusave jaman hela zinaenda kwa wenye nyumba. yaan tunafanya kazi kulipa Nyumba hili ji Jipu Pia litumbuliwe kama wanavyotumbua shisha na Mashoga. na hili nalo la nyumba yaan ni kero hasa" Diva Loveness
DIVA Loveness Amtaka Paul Makonda Awatumbie Wamiliki wa Nyumba za Kupanga Mjini
2
July 16, 2016
Tags
Jenga yako kwa mkopo uone kama utapangisha kwa bei ya kutupa wakati mkopo unakungoja. Nakubaliana na wewe kuwa hakuna haja kulipa 6 + months yawezekana rent ya mwezi tu. Ila wapangaji nao ni kero utakimbizana nao kila mwisho wa mwezi na visababu kibao. .ooh nimefiwa. ohh naumwa ooh ada. Hata wenye nyumba wanahitaji Makonda awajibike wapangaji. TRA wakidai kodi kwa wenye nyumba rent itapanda pia. Maana mlipaji ni huyo huyo mnunuzi. Kazi ipo.
ReplyDeleteMiezi sita mbona michache. Nikijenga ni kulipa kwa mwaka kama unaona shida kajenge yako au tafuta chumba kimoja uswahilini. Nilifikiri mrembo kama wewe una nyumba yako tayari. Wabongo punguzeni matumizi yasiyo na ulazima ili muishi kulingana na vipato vyenu (budget)
ReplyDelete