DJ JOH wa 93.1 Marekani acheza Ngoma za Diamond!

Haya sasa naona taratibu ule ubishi wa kuwa nyimbo za Afrika hasa Tanzania hazichezwi kwenye vituo vya Radio za Marekani unaelekea kuisha!

Dj Joh wa 93.1 Marekani akihojiwa na Millard Ayo amezungumzia nafasi ya wasanii wa Afrika kusika katika vituo vya Radio vya marekani!! Amelezea Mengi lakini amekiri mara ya kwanza ili apate hiyo kazi ilibidi adanganye na alikataa kuwa yeye si mtanzania kutokana na ubaguzi lakini baadae alikuja kukubari kuwa ni mtanzania baada ya kazi zake kuanzwa kupendwa! Alienda Marekani kwa ajiri ya kusoma lakini alifika hatua akaanza kuwa Dj lakini hakuruhusiwa kuplay nyimbo za kiafrika kwani hakuwa anaruhusiwa!!

Anasema yeye ni anapenda Afro Pop na anaupenda sana mziki wa Diamond!!!! Kwa mara ya kwanza alijitosa na kuanza kuplay nyimbo za akina P-squre,Wizkid na Diamond!!! Anasema siku hiyo alipokea comments nyingi sanaaa zilizo mpongeza na kufanya yeye kuongeza juhudi ya kuplay nyimbo za kiafrika hasa Za diamond

Anasema siku ambayo hatoisahau ni siku Alio play nyimbo za Diamond na baada ya kipindi alipigiwa simu na Mtu ambae ni Mmarekani na alimuuliza kuwa Diamond kamfahamia wapi ndipo Dj Joh alipo sema yeye ni mtanzania na anamfahamu Diamond!!! Yule mmarekani alimwambia yeye Kwa Afrika Diamond ndo Msanii anaye mvutia na kwenye Gari yake muda mwingi huwa anasikiliza nyimbo za Diamond japo haelewi lugha!!! Dj Joh amesema kuwa Yule mmarekani alimwambia wiki ijayo nina harusi yangu na ninaomba uje Uwe Dj kwenye Harusi yangu na Nyimbo za Diamond uwe nazo nyingi!! Hapo Dj Joh anasema alifurahi nakuona kuwa mziki wetu sasa unakuwa!! Dj Joh amesema number don't lie kwani ni wengi walio mpigia simu na kumpongeza na kumtaka kumjua Diamond!!!

Mbali na hilo kuna siku Diamond alipost video ilionesha sehemu fulani Marekani watu wapo kwenye shuhuri wakisikiliza Nasema nawe!! Millard ayo ameongeza na kusema kuwa pia kuna kituo kingine cha Radio marekani kinachoitwa CSB nacho hucheza nyimbo Za Diamond!!!

Ni wazi sasa mziki wetu umefika mbali!!! Kuna siku niliwahi sema Diamond nyimbo yake na Neyo itachezwa sana kwenye Vituo vya Radio vya Marekani lakini watu walinipinga sana humu na sasa limeanza kujidhihirisha Kabla hata ya hiyo collabo

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Sahihisho kwa mwandishi:
    Kukubari - kukubali
    Kwa ajiri - kwa ajili
    Shuhuri - shughuli

    ReplyDelete
    Replies
    1. Asante sana mdau wa hapo juu July 18,2016,11:19 kwa kumsahihisha huyo mwandishi wa hizo habari za hapo juu yaani ni kweli kabisa kuwa watu wanakera sana jinsi walivyokuwa hawakijui kiswahili wakati wao ni wabongo na wameenda shule lakini bado lugha yao inawapiga chenga yaani inaudhi kweli kweli kusoma makosa kila siku mitandaoni mpaka haileti raha nakumbuka sana wakati bado ninasoma mwalimu wetu wa somo la kiswahili aliwahi kutuambiaga kuwa lugha ya kiswahili ni ngumu sana japo wengi huichukulia lugha hii kuwa ni poa wakati sivyo hivyo kabisa tunayaona makosa ya lugha kila siku mitandaoni kweli kabisa nayaamini maneno ya yule aliyekuwa mwalimu wangu wa somo la kiswahili wakati ule ninasoma shule ya Tambaza secondary school/1978 old school

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad