Dk. Kigwangalla ametoa taarifa hii kuhusu wanaosapoti mapenzi ya jinsia moja

Ishu ya watu ambao wanashiriki mapenzi ya jinsia moja imekuwa kubwa kiasi kwamba viongozi mbalimbali wamekuwa wakizungumza katika maeneo mbalimbali ambayo wanapata nafasi ya kuzungumza na kukemea vitendo hivyo.

Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla ameendelea kusisitiza kuhusu vitendo hivyo na kueleza kuwa serikali haipo tayari kuona vitendo hivyo vinafanyika kwa wananchi wake lakini pia kuzitangazia mwisho wake taasisi ambazo zinafanya jitihada kutetea watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.

Dk. Kigwangalla ametoa taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa Twitter ambapo aliposti video ambayo ikimwonyesha akikemea vitendo hivyo na kusema kuwa serikali itazifutia usajili mara moja taasisi zote ambazo zitabainika kupokea pesa kutoka mataifa ya nje ili kutetea mashoga.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Akome ana nini
    Naye mavazi yake tu mwenzetu haachi

    ReplyDelete
  2. Aka. Dr K
    Huna kioo
    Mavazi uvaayo
    Mwendo utembevyo
    Hallo
    Macho hawana vipofu
    Maskio hawana. Viziwi
    Midomo hawana mabubu
    Hata pua hawana ya kunusa umwenzetu
    Acha hiyana madaraka yanapita
    Lakini asili na jadi yetu tunakufa nayo
    Aka mwenzetu huachiiiiiiiiu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad