BAADA ya Serikali kukifutia usajili Kituo cha Tiba Asili cha ForePlan cha Dk. Juma Mwaka, hivi sasa amekigeuza kuwa kampuni inayojishughulisha na bidhaa za afya, usafi na urembo.
Julai 12 mwaka huu, Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala ilivifutia usajili vituo vitatu vya tiba asili kikiwamo cha ForePlan kwa madai ya kukiuka taratibu za kitabibu za tiba asili, huku wakiwa wameonywa lakini walishindwa kubadilika.
Sababu nyingine ya kufungiwa kliniki hiyo, Serikali ilisema katika matangazo ya kituo chake, Dk. Mwaka alikuwa akitangaza kuwa anatoa tiba za kisasa huku akiwa hana elimu inayomruhusu kufanya hivyo.
Akizungumza na Kituo cha Redio cha Clouds FM Julai 15, mwaka huu, Dk. Mwaka aliwataka Watanzania kuwa tayari kupokea bidhaa zitakazokuwa zikisambazwa na kampuni yake ya ForePlan.
“Ninachoweza kusema ni kwamba kaa tayari kwa bidhaa ya FP ambayo itakuwa adimu, watu wanaoijua wameanza kuitolea oda, kwa bahati nzuri imesajiliwa ndani na nje ya nchi,” alisema Dk. Mwaka.
Aliwataka wafike ofisini kwao na kupata maelekezo sahihi wanayoyahitaji na kwa watu wa mikoani watapata huduma zao kwa kupiga namba za simu 0767600600 na 0762 400400, hivyo watapata bidhaa zao huko walipo.
“Unapozungumzia afya, urembo na usafi, unazungumzia Kampuni ya ForePlan, ofisi za kampuni zinapatikana Ilala Bungoni Dar es Salaam, ukifika Ilala ulizia ForePlan na hata ukimuuliza mtu kwa jina maarufu kwa Dk. Mwaka atakuonyesha,” alisema.
“Unachotakiwa kufanya ni kutoa maelezo ya bidhaa unazozitaka na ambacho unakitaka, utapewa ushauri wa bidhaa za kutumia na ikiwa utachagua kutumia bidhaa za forePlan, utapewa gharama za bidhaa hizo halafu ukishatuma fedha kwa njia ya M.pesa utatumiwa bidhaa huko uliko.
“Ninachoweza kusisitiza ni kwamba ukiongelea afya, urembo na usafi, unazungumzia kampuni ya ForePlan. Kwa hiyo usisite kuwasiliana nasi na kutembelea ofisi zetu zilizopo jijini Dar es Salaam au kutupigia kwa namba za simu ambazo nimekutajia,” alisema Dk. Mwaka.
mmmmmmmmmmmmmhhh
ReplyDeleteHahahahhahahhaha baba magu anazidi kufanya hali kuwa ngumu...yani ni checheeee
ReplyDeleteMhhhhhh...... urembo, afya na usafiii.... acha bwana.
ReplyDelete