Donald Trump Amsifu Saddam Hussein na Gaddafi...Adai Dunia Ingekuwa na Amani Kama Wangekuwepo

Mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump amemsifu kiongozi wa zamani wa Iraq Saddam Hussein akisema aliweza kukabiliana vyema na magaidi.

Bw Trump alikuwa akihutubia mkutano wa kampeni eneo jimbo la North Carolina Jumanne alioanza kuzungumza kuhusu kiongozi huyo aliyeuawa kwa kunyongwa Desemba 2006.

“Saddam Hussein alikuwa mbaya, kweli? … Lakini mnafahamu ni jambo gani aliweza kulifanya vyema sana? Aliwaua magaidi. Alifanya hivyo vyema sana,” Trump alisema.
“Hawakuwasomea haki zao, hawakunena lolote. Walikuwa magaidi, mambo yao kwisha.”
Trump: Dunia ingekuwa bora na Gaddafi na Saddam
Bw Trump awali amewahi kusema kwamba ulimwengu ungelikuwa “asilimia 100 bora kuliko sasa” iwapo viongozi wa kiimla kama Saddam Hussein na kiongozi wa muda mrefu wa Libya Muammar Gaddafi wangelikuwa bado uongozini.

Kabla ya uvamizi ulioongozwa na Marekani, ambapo Saddam aliondolewa madarakani, Iraq ilikuwa imeorodheshwa na Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani kama taifa linalofadhili ugaidi.

Saddam Hussein aliongoza Iraq kuanzia 1979 hadi 2003
Afisa mkuu mshauri wa Hillary Clinton kuhusu sera, amejibu matamshi ya Bw Trump kwa kusema kuwa: “Sifa za Donald Trump kwa viongozi wa kiimla yamkini hazina mipaka.”

Amesema matamshi kama hayo yanaashiria “ni jinsi gani itakuwa hatari (kuwa na Trump) kuwa Amiri Jeshi Mkuu na jinsi ambavyo hafai kuhudumu kama rais.

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kazi ipo
    Matamshi haya yanatuhusu nini watanzania ?

    ReplyDelete
    Replies
    1. utangoja sana yanayokuhusu.
      wewe soma tu.

      Delete
  2. Upotoshaji kiuandishi na kuziba uhuru. Ni mbinu za kibabe zinazoingia Tanzania ambapo huwezu linganisha na nchi za ughaibuni. Tanzania hatupo huko. Nyinyi waandishi mnaopendelea chama ni vipofu na mnatenganisha, gonganisha watu, na mnasapoti ubabe ambao nchi hii haihitaji hasha. Vichwa vya habari kama hivi vinawagonganisha wanasiasa. Inawalenga wapinzani mojakwa moja ambao wanatetea uwepo wa katiba kwanza, ili nchi iwe na sheria halafu kufuatana na sheria itende haki na nchi itendewe haki na watu wake. Nchi imeibiwa kwa miaka kumi. Tanzania ya sasa inajengwa mwa kuigwa, msukumo na mfumo wa nje bila kujali katiba nzuri ili imlinde mtanzania na mali ya mtanzania. Kuna uarabu hapa, uchina pale, umarekani huku na uingereza, ufaransa kule. Hawa wote wameingiza mizizi yao kwa muda huu wa miaka kumi kupitia uongozi uliopita Mtanzania tu ndiye anayebabaishwa ingawa ni nyumbani kwake. Lini watu mtaamka. Najua kila mtu anahangaika kutafuta pesa, kwa pamoja hakuna muungano kamili unaompa uhuru na nguvu kamili ili mtanzania ayaone haya yote na kuyatolea hoja. Ni kuzimwa kila siku. Mtanzania anakuwa less important nyumbani kwake wageni wanaiendesha na kuitawala Tanzania tena baada ya miaka hamsini ya uhuru. Ubinafsi wa viongozi awamu iliyopita. Lazima hii ipewe umuhimu mkubwa sana.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad