Haji Manara aanza kupata matumaini ya kuona


Kuna matumaini kwa Haji Manara atarejea na kuona kama kawaida baada ya matibabu yake jijini New Delhi nchini India.

Manara amezungumza  leo na kusema tayari ameanza vipimo na ana matumaini.

"Nimemaliza vpimo vya awali na kuonyesha matumaini ya kupona. Tayari nishaanza tiba na kesho natarajiwa kulazwa hospitali kwa siku tatu kwa uchunguzi zaid na matibabu.  

"Imani imekuwa kubwa kwa majibu ya leo, ambayo yanaonyesha kuvilia na kuganda kwa damu katika macho yangu.                           

"Madaktari wanasema upo uwezekano mkubwa wa kupona ila watajua zaidi baada ya kumaliza tiba ya awali na uchunguzi," alisema Manara.

Manara amesafirishwa kwenda India baada ya kuamka asubuhi jicho lake likiwa halioni kabisa huku moja likiwa limepoteza uwezo na kubaki kwa asilimia 10 tu.
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mungu ni mkubwa atakusaidia ili ueze kuona vizuri mimi pia nataka uweze kuona vizuri ingawa siko bongo na sijui ugonjwa wako lakini Mungu ni mwena kwa wote

    ReplyDelete
  2. Mungu akuponye

    ReplyDelete
  3. mtegemee mwenyezi Mungu kwa kila jambo utapona tu bro!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad