Hii Ndio Jinsi ya Kuepuka Kuwa Mchepuko

Mara nyingi asilimia kubwa ya wanawake hupenda kuwa na wanaume wanaojiweza kiuchumi. Lakini baadae wanapotambua kwamba mwanaume huyo ameshaoa hushangaa sana, huumia na kusema waliwaamini kuwa wako single na kwamba wanaume wote ni mbwa tu.

Wanaume sio mbwa au paka shume, ni nyie wenyewe ndio mnashindwa kuwaelewa na hamtaki kufanya uchunguzi. Mlishaambiwa kwamba nyuma ya mwanaume mwenye MALI na MAFANIKIO kuna mwanamke. Na wewe unataka mwanaume aliyefanikiwa. Unategemea nini?

Kama utakutana na mwanaume ambae ni handsome, ana mali, anaendesha gari nzuri, yuko vizuri kiuchumi, basi huyo sio mumeo mtarajiwa, huyo ni mume wa mtu fulani kwa muda huo. Ni agharabu sana kukutana na mwanaume anayejiweza halafu akawa single, either uwe shareholder au unyang'anye share zote za mwanamke mwenzako kitu ambacho sio busara hata kidogo.

Mume wako mtarajiwa yupo anahangaika kutoka na maisha, anapigania ndoto zake. Huenda yupo shambani, yupo dukani, anapiga kitabu chuo, au yupo anabeti. Kimsingi yupo anapigania kuchomoka kimaisha. Anakusubiri tu wewe umpe support na back up ya kutosha.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hahhahaha safi sana muandishi wao wakiona mwanaume katika gari safi kali kapendeza ananukia wanadhani yupo tuuu...huwa tupo kufanya hayo yote mpaka akanawiri nakufanikiwa hivyoo afu nyie ndo huwa mnajisogeza..

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad