Je, Huu Ndio Mwisho wa Siasa za Maigizo Toka UKAWA?

Kama picha inavyoonyesha hapo juu, hii inaonyesha kuwa UKAWA wanachokiongea na wanachokitenda ni vitu viwili tofauti. Labda ndio maana hata Rais ameamua kupuuzilia mbali malalamiko yao.

Huyu huyu Msigwa ndio alikuwa wa Kwanza kupinga fedha za bunge kwenda kutengenezea madawati, lakini leo ndio amekuwa wa Kwanza kupiga picha mbele ya madawati yale Yale aliyoyapinga.

Lini UKAWA walitengua kauli yao kuhusu kutoshirikiana na Serikali ya CCM achilia mbali Naibu spika.?

Je kuna haja ya kuendelea kuwaamini UKAWA,?Au wabunge wamechoka kuburuzwa na Mbowe bila hoja za msingi.?

Hongera Msigwa kwa kuonyesha unafiki wa UKAWA.

Source:Jamii Forums

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mwandishi hujaeleweka,na picha ya madawati iko wapi hapo?

    ReplyDelete
  2. Mnafiki wewe mwandishi
    Fedha si za ccm wala TULIA
    Zilikuwa za bunge acha unafiki na uzushi

    ReplyDelete
  3. mwandishi tumia akili ya kawaida tu kufikiri, fikiria zaidi

    ReplyDelete
  4. Yaani wewe mwandishi ndio kilaza wa mwisho kabisa. Ni jukumu la serikali kutoa huduma za kijamii kwa wananchi wake ikiwemo sekta ya elimu kwa ujumla. Kazi ya bunge ni kutunga sheria na kusimamia serikali. Bunge kutoa madawati ni kujipendekeza.

    ReplyDelete
  5. unapotoa comment tumia akili sio tope, inaonekana unachukia amani katika nchi hii

    ReplyDelete
  6. Udaku ukitaka wananchi tutoe maoni kwenye blog yako tusiruhusu watu'anonymous' kutoa maoni yao, au udaku ni udaku kweli? Kama hivyo twambie tuache kutoa maoni kwenye blog yako. Tungetaka jina na sura.

    ReplyDelete
  7. MWANDISHI KUSUDI LAKO NI NINI??

    ReplyDelete
  8. mwandishi wa habari endelea kujitekenya,watu wanajua wanachokifanya.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad