Je, Kuna Madhara Msichana Akifanya Mapenzi Wakati Akiwa Katika Hedhi (Siku zake)?

Kufanya mapenzi wakati msichana yuko katika hedhi hakuna madhara yoyote kiafya kwa mwanaume wala mwanamke kama kati yao hakuna mwenye ugonjwa wa zinaa.

Ila kama mmoja wapo ana ugonjwa wa zinaa, huo ni wakati wa hatari sana kwa maambukizi, kwa sababu utando ndani ya mfuko wa uzazi unabomoka na mlango wa mfuko wa uzazi unakuwa wazi. Hivyo ni rahisi sana vijidudu vya magonjwa mbalimbali kuingia mwilini mwa msichana. Vilevile kama msichana tayari ameambukizwa na magonjwa ya zinaa, katika damu yake viko vijidudu vingi vinavyoweza kumwambukiza mvulana.

Kwa sababu mara nyingi ni vigumu kufahamu kama kati ya wapenzi hakuna mwenye ugonjwa wa zinaa, haishauriwi kujamii ana wakati wa hedhi na kama ndivyo basi kondomu itumike.

Katika jamii nyingi kujamii ana wakati mwanamke yuko wenye hedhi haikubaliki kwa sababu ya mila au dini.
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. KINYAAA BHANA!

    ReplyDelete
  2. Maadili ya dini ya kiislam inakatazwa kufanya tendo la ndoa ikiwa mwanamke yuko kwenye hedhi(siku zake)ni madhara ya kiafya.

    ReplyDelete
  3. Huyu aliyeandika hii mada ana ukaribu mkubwa sana na baba yake ambaye ni shetani!! maandiko yamekataza na ukisoma Biblia walipokuwa wanapewa amri enzi za nabii Mussa, mwanamke akiwa kwenye hedhi haruhusiwi kujichanganya na watu na baada ya hedhi anatakiwa aoge vizuri, afue nguo zake na anyoe mav..i ndipo ajichanganye. Na mara nyingi mwanamke akishiriki tendo la ndoa wakati wa hedhi atapata matatizo makubwa ya kuumwa tumbo na sehemu hiyo kwenye kipindi hicho kunatanuka sana!! Na mwanaume anaependa kutembea na wanawake kipindi hicho uwa wanaugua sana tumbo (ngiri) na hata mabusha, na wakati mwingine sehemu ya kukojolea inaziba!! sasa wewe umetokea wapi uanepotosha watu.. Pumbavu zako...

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad