Jeshi la Polisi Lapewa Siku 90 Kuhakikisha Mitambo ya LUGUMI Inafanya Kazi Vituo Vyote

Jana akihitimisha bunge, naibu spika ametolea ufafanuzi utekelezaji wa mfumo wa kielektroniki wa utambuzi wa alama za vidole(AFIS), hoja iliyojengwa kutokana na mkaguzi wa hesabu za serikali(CAG) kwa kutokamilika kwa mradi huo.

Agizo la bunge lilimtaka afisa masuhuli wa jeshi la polisi kuhakikisha mfumo wa AFIS unafanya kazi ndani ya kipindi cha miezi sita. Ripoti ilieleza mfumo wa AFIS ulikuwa unafanya kazi katika vituo 14 pekee kati ya vituo 108 hivyo agizo la kamati halikuwa limetekelezwa kikamilifu.

Spika ametoa agizo kwa serikali kuhakikisha mfumo huo unafanya kazi ndani ya miezi mitatu ili kuboresha uwezo wa jeshi la polisi kuwa na utambuzi wa haraka wa wahusika wa matukio ya kihalifu katika vituo vyote nchini. Pili masuala yote yaliyobainika kuwa na dosari za kiutendaji yapatiwe ufumbuzi haraka.

Spika anatarajia sasa suala hilo litafikia mwisho na mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali atafunga hoja yake baada ya kujiridhisha na utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad