Julius Mtatiro: Kwa Uwazi Kabisa Nasema Hii ni AIBU KUU Kwa Taifa la Tanzania

Tunatangaziwa kwa mbwembwe kuwa Taifa letu linaenda kujifunza Teknolojia kutoka Rwanda. So shameful! Taifa ambalo limeshiriki kupigania uhuru wa nchi karibia zote za Afrika. Taifa lenye mamia ya MAPROFESA na wataalamu wa Teknolojia za kila namna. Kwa hiyo hawa MAPROFESA wetu tunaowalipa mamilioni ya mishahara kwa mwezi, tena waliosomea teknolojia mbalimbali Uchina, Urusi, Marekani, Ujerumani, Uingereza na kwingineko (kwenye vyuo vinavyoheshimika duniani) ni Maprofesa UCHWARA! Tatizo la nchi hii ni kubwa hadi mkuu wetu hajua tutaanzia wapi. Kwa uwazi kabisa nasema hii ni AIBU KUU!
Mtatiro J

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mtatiro Je Si umesikia Lipumba Ni plofesa

    ReplyDelete
  2. Mtatiro...hasha Si kweli Ni ufinyu WA uelewa wako.

    ReplyDelete
  3. Wewe aikuzote iko jirani ya plofesa..je sasa unataka kumtukana au kweli Uchwara

    ReplyDelete
  4. Bwana Julias. Nashukuru sana kwa maoni yako. Tanzania kuna wasomi wengi na wazuri ila wengi wao wameikimbia Tanzania. Sababu ni kwambwa:
    Nchi yetu kuna maneno mengi ( Siasa za uongo.) Fitina kibao,kujuana kwingi,maonevu kibao na mambo mengine mengi siwezi kuyaandika nikayamaliza. Njoo hapa USA utakutana na madaktari wazuri kutoka Tanzania, maporofesa wa zuri kutoka Tanzania, na wafanyakazi wengi wa zuri kutoka Tanzania ukiwauliza kwanini hawataki kuridi kufanya kazi nyumbani wanakwambia kuwa Tanzania niyawenyewe.

    ReplyDelete
  5. Ukweli ni huo hawa wanaoitwa wanataaluma waliobobea ama maprofesa wa Tanzania hawana jambo lolote jipya sana zaidi ya kufanya ulevi, uzinzi wa kupindukia pamoja na kujifanya wanasiasa uchwara. Kimsingi wasomi wengi wa kitanzania hawana dhana endelevu katika taaluma zao. Wakiisha maliza masomo ndio imetoka vitabu na akili zote wanaziacha chini ya uvungu wa kitanda.

    ReplyDelete
  6. Kuna ubaya gani kujifunza kutoka Rwanda. Raisi wa Rwanda anajari watu wake, kule kuna nidhamu ya hali ya juu, nenda Kigali ukajifundishe usafi unavyo fanywa!!!

    ReplyDelete
  7. Tanzania haithamini wasomi.Tanzania ni uhusiano kindugu bila elimu.
    Ubinafsi wa viongozi kindugu, kirafiki na kuwasakama wasomi, kuwweka ndani, kuwanyanyasa na kuwanyima ajira. Anayefaidi Tanzania lazima awe mwana ccm, mtii, asiyehoji mambo, asiye na fikra, na anayejali pesa tu.wao pesa ni maendeleo elimu haina faida, pesa kwao ni maendeleo.
    Ukitafakari matajiri wengi wakuu wa Tanzania ni wanasiasa ambao hawajui namna ya kufikiri nje ya siassa na hawana utaalam wa ubunifu kikazi.kama mnaliona hili tatizo angalieni mfumo wa siasa nchini. Huruhusiwi kudadisi, huwezi uliza vigogo wameyajengaje majumba makubwa kutokana na mshahara mdogo wanaoupata. Huwezi uliza ni nani alipitisha makonteiner. Huwezi uliza namna gani mashine hayakufungwA ingawa pesa ni za umma, unamwachia mtuhumiwa ajitetee. Rwanda sasa itafanikiwa zodi ya Tanzania, kagame msomi anajua viongozi wetu fikra fupi, anachukua mwanya huu kuifaidia nchi yake na watu wake. Tanzania imeoana na Rwanda sasa. Mnaona wanaukawa wanayaelewa haya mambo, lakini wanazimwa na wasiojua kufikiri, na wasioona mbi, wasiokaa nchi huru hawaewi bado.
    Haya mambo no wenyewe watanzania mnayakubali. Wengi visomo vya kubabaishia tu. Hata tukipewa mwanya wa kuendelea bado tupo kama kondoo.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad