Kambi ya aliyekuwa Mgombea Urais wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kwa tiketi ya Chadema, Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowasa imemfungukia muigizaji wa Bongo Movie, Jacqueline Wolper, siku chache tu baada ya kutangaza kurejea Chama Cha Mapinduzi (CCM) mjini Dodoma.
Wakizungumza na Risasi Mchanganyiko kwa nyakati tofauti juzi jijini Dar es Salaam, wasemaji wa kambi hiyo walisema alichokifanya Wolper ni utashi wake wa kisiasa, unatokana na hisia zake, ingawa pia walimsema kama mtu asiyefahamu misingi, sera, itikadi, imani wa ilani za Chadema.
Msemaji binafsi wa Lowasa, Aboubakary Liongo, aliliambia gazeti hili kuwa ni vigumu kwa kiongozi huyo kumzungumzia Wolper kwa sababu hakukuwahi kuwa na ‘connection’ ya moja kwa moja baina yao, isipokuwa msanii huyo alijiunga na wanamabadiliko kwa utashi wake mwenyewe.
“Mzee hawezi kumzungumzia, alikuja huku kama ambavyo vijana wengine wengi walikuja wakifuata mabadiliko, kama kuna wa kumzungumzia, labda ni viongozi wa chama kwa sababu operesheni zote zilizokuwa zikifanywa wakati ule, ziliratibiwa na chama.
“Wao ndiyo wanaweza kuwa na la kusema kuhusu yeye, ila ninachokiona mimi ni kuwa Wolper ni mtu mzima, mwenye akili timamu, alikuja kwa utashi wake na kama anaondoka, pia anafanya hivyo kwa utashi wake,” alisema Liongo, ambaye ni mtangazaji mwandamizi wa redio nchini.
Kwa upande wake, msemaji wa Chadema, Tumaini Makene, alisema Wolper ni mtu asiye na msimamo, asiyeelewa misingi, ilani, sera wala itikadi za Chadema, ndiyo maana haelewi nini anafanya.
“Sisi tuko na watu wanaoishi kwa matendo, siasa ni maisha ya binadamu, mtu ‘siriaz’ anajua misingi, itikadi, falsafa, imani na ilani za chama chake, hawezi kuwa leo anaamini hivi kesho vile, ukiona mtu kama huyo, ujue hana msimamo, anayumbishwa na ni mtu anayefuata mkumbo,” alisema Makene.
Lowassa 2Aliyekuwa Mgombea Urais wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kwa tiketi ya Chadema, Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowasa
Msemaji huyo alitolea mfano wa vyama viwili vikubwa vya siasa nchini Marekani, Republican na Democrat, akidai waumini wa taasisi hizo mbili za kisiasa, ni watu wenye weledi wanaojua nini wanafuata, hivyo siyo rahisi kuona mtu akihama ovyo kutoka upande mmoja kwenda mwingine.
Wolper ambaye aliwahi kuwasuta waigizaji wenzake walioamua kujiunga na CCM kwenye kampeni za uchaguzi mkuu uliopita, akisema ni watu wasioitakia mema taifa kwa kushindwa kuungana ili kulikomboa, hivi karibuni alitangaza kurejea chama tawala, akisema anarudi nyumbani kwani alipotea njia.
“Nimerudi na sifikiri tena kugeuka nyuma, nimeona jinsi rais wetu anavyopigana na chama hiki kuwakomboa wanyonge na sasa hivi kina kasi ya ajabu na nitaendeleza niliyoyaacha,” alisema msanii huyo wakati wa hafla ya kumuaga Mwenyekiti Mstaafu wa CCM, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete mjini Dodoma.
SI MUMUACHE!
ReplyDeleteKILA MTU NA MAISHA YAKE.
Biashara gani hasa. Ya kuwapamba wazee wa vyama? Hajielewi. Uchangudoa wa kusiasa tu.
ReplyDeleteHayo ni maneno ya mkosaji,Wolper ndo kashaamua mwacheni mtoto wa watu jamani,kaona mwelekeo wa TZ ni mzuri ingawa UKAWA bado wanachonga,kwa nini asiamini UKAWA ni wapenda madaraka tu?Nchi ina adabu hata mwaka bado.HAPA KAZI TU.
DeleteLiongo ameeleza kwa busara kuwa wolper ana utashi wake wa kuwa kule anakoona kunamfaa.Makene unakosea unaposema hana msimamo maana hata walioko sasa Chadema walihama toka CCM, je nao hawana msimamo? Msimamo ni muhimu lakini unamsema wolper kuwa hana msimamo jua kwa namna moja unawasema waliohamia chadema!
ReplyDeleteyuko sahihi kuhamia kokote anakotaka kwenda
ReplyDeleteMnyonge mnyongeni lakini mpeni haki yake and that's it
ReplyDeleteTangu lini MALAYA akawa na KITANDA
ReplyDeleteNawashangaa hao viongozi wakuu kumpokea kwa vishindo
Kumbe Lowassa bado tishio CCM
huyu mwanamke alibadili dini kutoka mkristo kwenda mwislamu,alafu akarudi tena kwenye ukristo,jamaa yake wa sasa ni mwislamu usishangae akarudi tena kuwa mwislamu,sasa wa kumjadili kweli huyo?na anaushawishi ganikatika jamii?jamani tuache utani tujadili mambo ya muhimu.
ReplyDeleteWolper kawauma sana kuhamia CCM,Sasa bado kuna mmoja nae yuko njia moja kurudi CCM ndio hamtaamini na mapovu yenu hayo.
ReplyDeletewewe kapimwe akili zako kilaza kweli wewe.
DeleteKASHTUKA!
ReplyDeleteNg'ombe aliye kosa mkia ndani ya zizi. Period
ReplyDeleteLowassa kweli ni tishio
ReplyDeleteBongo
Regina mtunze mzee wetu
Kila kukicha hawalali mzimu wake bado na bado
Makene hilo ni dongo kwa Lowasa na Sumaye, hawana msimamo......hahaha FIKIRI KABLA YA KUSEMA.......peopleeeeeezzzzz PWAAAAAAAA
ReplyDeleteKoma mwana kukoma
DeleteYa Lowassa na Sumaye
Uwalingslishe na Malaya huyu
Fyuu
Lowassa wala Sumaye hawana njaa waliondoka ccm baada ya kufanyiwa zengwe
Na hili Malaya lisilokuwa na KITANDA tena kupokelewa na mwenyekiti mikutano mkuu
Alipogama yeye na Malaya wenzie walio rudi jinsi walivyokanda ccm
Leo mnawapokea ccm again
Lowassa wala si Sumaye hawaumiii kwa hili ili sisi watanzania tunawashangaa ccm
Mmekosa nini
Mkutano mkuu mzima issue Lowassa na Sumaye
Fyuuuuuu
Kweli chama cha mafisadi ccm
Huyu Malaya aso KITANDA anacheza Dili fyuuuuu
ReplyDeleteCCM
Anzisheni kozi kabla hujawa mwanachama
Mtajuwa makapi na wasaliti Nani tena kbl ya kupewa uanachama tangazeni
Kama vile kuomba uraia
Hapo mtajuwa
Angalia chini Malaya huyu
"Sikuwahi kuwa na kadi yoyote ile ya UKAWA na sasa hivi nimeamua kuingia CCM na sijashawishiwa wala kuhongwa, hakuna mtu amenivuta shati kuingia CCM, nimeona kile kitu nilichokua nakitaka kwenye nchi yangu Mhe. Magufuli anakifanya sasa, naipenda CCM na CCM ni nyumbani"-Jackline Wolper
Nini maoni yako kuhusu kauli hii ya Jackline Wolper?
Ff
ReplyDelete