Kauli ya CHADEMA baada ya wanachama wake kutangaza kujiunga CCM

Wakati wa Mkutano Mkuu wa CCM jana mjini Dodoma, Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA) kiliwapoteza wanachama wake watatu baada ya kutangaza rasmi kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Wanachama hao waliokihama chama hicho ni Fred Mpendazoe ambaye alikuwa mwanachama wa CCM pia aliwahi kuwa Mbunge wa Kishapu mwaka 2005 hadi 2010 kupitia CCM, Mgana Msindai aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida na mbunge wa zamani wa Iramba Mashariki na mwigizaji wa filamu nchini Tanzania Jackline Wolper.

Mmoja wa wajumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA alipohojiwa jana wakati kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho kinaendelea alisema kuwa, hawana muda wa kukaa na kuanza kumjadili mtu mmoja mmoja anayesemekana kuhama chama hicho.

"Kamati Kuu ni kikao kizito sana, hatuwezi kuacha kujadili masuala ya msingi na kuanza kuwajadili hao wanaosemekana kuwa wamehama chama," alisema mjumbe huyo.

Kamati Kuu ya CHADEMA imekutana jana na leo katika vikao vya dharura ikiwa na lengo kubwa la kujadili mwenendo wa hali ya kisiasa nchini.

Post a Comment

12 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Chadema hatuzungumzi juu ya wacheza mpira
    Ambao hujiunga na club only kwa ajili ya pesa
    Hayo wanataweza ccm
    Chama cha mafisadi CCM
    Hata initial zake sawa
    Tena na wote waliokuja kwa kufuata mtu au watu watoke warudi ccm
    Chadema haitakufa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sasa Lowasa aliyekuja kwa kufuata cheo(urais)tena kwa kununua unamuweka au yuko upande gani?nae si mcheza mpira?

      Delete
    2. mburura wewe mshenzi, nani analea mafisdi kama si nyinyi chadema??? huro fisadi papa lowasa na huyo anayekwenda kugombea wilaya wakati alishawahi kuwa waziri mkuu mfyuuu pumbavuuuu

      Delete
    3. CCM ndio baba yako,kazaliwa na babu yako TANU,
      Haiingi akilini kukiita chama cha mafisadi wakati mgombea wenu katoka huko ccm na ndio mnamkumbatia,Yaani bora haya wayaseme vyama vingine lakini sio CHADEMA.Wenye kuona mbali washasema kuing'oa CCM madarakani labda YESU arudi.Habari ndio hiyo,HAPA KAZI TU!

      Delete
    4. Koma wewe tulikuwa na chama kimoja
      ccm ni mama yangu wala baba shenzi pumbavu

      Delete
    5. Fisadi mkuu si mnaye nyie chadema tena mlimpokea kwa mbwembwe zote mkampa nafasi ya juu kabisa ya kugombea uraisi.ama kweli bora unyimwe vyote lakini si kuto kujitambua.

      Delete
    6. Baba yako mwenyewe na mnaokula kupitia ccm.... nyama weee Lowasa atawatoa rohoooo, mnaumwa kwa ajili yake. Peoples Powerrr

      Delete
  2. Watu wengine wanafuata ushabiki na ukabila/ukanda tu,hawana muda wa kuchunguza kwa undani,hiki ndicho kilichomkuta dada yetu Jack.

    ReplyDelete
  3. Jack ameshawishiwa na hao wasafi family maana ni ccm na yeye anataka penzi ilibi arudi ccm hakuna cha zaidi hapo. Na inaonekana Lowassa anawauma roho vibaya, mtaisoma namba mbona Mzee Kingunge alishaiona ccm bure kabisa.
    huko ccm ni kujuana tu oh, huyu wa siku nyingi ndiyo anapewa cheo, na vimemo kwa kwenda mbele... Aluta continua a.k.a. mapambano bado yanaendelea.

    ReplyDelete
  4. Kosa kila kitu pata Akili. Utaichukua kokote duniani uendako. Lakini Watanzania wengi wavivu wa kufikiri, niseme utashi mdogo. Mtanzania ukimpa sukari kuilamba atasahau kila kitu. Nchi ipo njia panda. Ufisadi bado upo mkubwa tu na wa hali ya juu kupitia gesi, ardhi, madini. Huku kote bado CCM haitaki kuachia sababu ndiko pesa za investment kubwa za Wananchi wenye mali hizi zimechukuliwa au kutaifishwa kinyume cha sheria na vigogo wa nchi hii. Huko ndiko chimbuko la mauaji ya tembo,biashara ya ndovu, vibali vya kuwinda wanyama hao vinamilikiwa nao na shemeji zao. Huko ndiko Watalii walipao mamilioni kwa wiki ndiko waendako. Badala ya kugawa , kupima viwanja hivyo na kuwakabidhi Wamassai, wamewafukuza na kuwapa hawara zao.Tuliimba nyimbo kali, JKT, POlisi, Wanafunzi, Wananchi kwenye kila tamasha enzi za uzalendo na kuwatukana vibaraka, Makaburu, mabepari. Na wengi hawa viongozi waliokiuka leo wengine walikuwa jeshini, shuleni au kwenye jamii zilezile zilizolaani. Leo tunashindwa kuwauliza, Kuwazuia, kuwapeleka mahakamani. Wanadai tunahitaji Wawekezaji, Mwekezaji hawezi kuinua nchi isiyo ya kwake, ataitumia kwa faida yake mwenyewe na kukuacia magonjwa, mazingira mabaya, atakunyanyasa. Mwekezaji kahujumu nchi sababu wenye nchi na ardhi hii kufuatana na sheria za nchi hawakuhusishwa katika utoaji wa mali hizi. Sheria za Tanzania na Ulaya ni tofauti. Watanzania tukiungana kutafuta haki tutashinda tu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. nosense kubwa sima hata uandishi ni fake punguwani mkubwa we anony 11.11pm

      Delete
  5. Afadhali mi punguani kulipo debe tupu. Haa.
    Kila kukicha linatika.Mwangalieni Trump. mpaka anatoka mapovu. He is such a small person. Ukali usiona akili, bubuja maneno kesho anajisahihisha, pupuru papara, hana wala hasikii ushauri. Anakemea mpaka jasho linamtoka. Lakini wenye akili wanaujua udhaifu wa Trump.ni beng beng isiyoisha ni Aibu kwa Taifa la Marekani, Amefikaje hapo, wengi walilaza akili hawamkuchukulia maanani.
    Pole kaka.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad