Mgomo wa daladala Jijini Mwanza umesababisha kijana mmoja Jijini humo kutamka lugha chafu ndani ya gari ambayo alipewa lifti limemsababishia kuishia mikononi kwa sheria.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi akizungumza katika kipindi cha East Africa Breakfast dereva wa wa gari likitoa lifti Hassan Bushagama mkazi wa Buhongwa Jijini Mwanza asema alipofika eneo la Buhongwa akiwa na usafiri wake aina ya Toyota Noah kutokana mgomo wa daladala aliamua kutoa lifti kwa abiria aliowakuta hapo.
"Walipanda watu kama nane ambapo Dada mmoja akasema watu walivyo hawatakawia kusema Rais Magufuli ndiye anatakiwa aulizwe,kijana mmoja wa umri wa miaka kama 27 au 28 hivi akadakia akasema Rais ni '******** 'mzee mmoja akamwambia kijana tengua kauli lakini akakataa na kusisitiza ,abiria wakataka kumpiga nikawaambia mwacheni tumpeleke 'polisi " Amesema Bwana Bushagama.
Bushagama ameendelea kusema kwamba "Baada ya hapo niliendesha gari langu hadi kituo cha polisi tulipofika pale nikawaambia polisi hali halisi askari akawahoji abiria wakaelezea hali hiyo na yeye alipoulizwa akasema ,amesema hivyo lakini hakujua kama ingepelekea kufika huko.
Aidha Bushagama ameongeza kuwa wameamua kusitisha kazi zao na kuonesha uzalendo ili kuonesha kwamba Rais hawezi kutukanwa namna hiyo.
Kwa upande wake Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Mwanza Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kwama kijana huyo amejitetea na kusema kwamba alisema alimaanisha wanaogoma wanajifanya wapumbavu lakini Rais ni ******** zaidi yao jambo liliwakasirisha wenzake na kuamua kumfikisha kituo cha Polisi.
Kamanda ameongeza kuwa suala hilo tayari limefikishwa Polisi kitachoendelea ni ushahidi ukitosheleza kijana huyo atapelekwa mahakamani.
Vitu vingine vya kipumbavu
ReplyDeleteKamanda mzima wa polisi kuzingumizia ya watu vichaa
Unapokuwa kiongozi popote duniani
Kutukanwa kwa aina hii si Jambo la ajabu
Hata Obama, papa hutukanwa na vichaa
Hawa waliompeleka kijana huyu pia wanahatia.Namuomba tena Raisi Magufuli kama ni mtu mcha Mungu amtoe huyu kijana.Mkiangalia ukweli wa mambo, huwezi kumkatisha kijana au mtanzania yeyote maisha yake kwa jambo kama hili.Raisi Mkapa alitukana wananchi hadharani wala sheria yeyote hakufanyika. Raisi Kikwete pia, na nimewasikia viongozi wa CCM wamefanya hivi juzi Dodoma.wewe uliyempeleka kijana huyu polisi nakuomba sana fikiria jinsi unavyomkatisha huyu kijana wa watu maendeleo yake.wezi wa mamilioni wapo bado wanavyeo vikuu serikalini, waliosafirisha meno ya tembo wamebaki kuongoza chama cha ccm, .ukilinganisha nani anachukuliwa hatia nani hachukuliwi hatua kutokana na makosa yao hayaendani hata..Ukiwa raisi wengi watakupenda wengi hawatakupenda inabidi ukubali hili.Hata raiso mwrnyewe aliwaita watu vilaza je hili si tusi. Inabifi raisi Magufuli ajiulize alipoingia uraisi hakuja kunga watu.Yesu alitukanwa kazi yake ilikuwa kusamehe hao na kusema hawajui walitendalo.je Ndugu Magufuli ni mtakatifu?anaposikia haya inabidi aongeze utukufu wa kufanya kazi kuwatumikia watu.kama ulivyotolewa mfano na Makamba ingawa sikubakiani naye mengi, raisi ni mtumishi si mnyapala. Anavyoitika nena bwana ntumishi asikia mtumishi gani anakubali maisha ya vijana yafanyiwe hivi.yeye mwenyewe kama ni kweli aliukataa utumishi na akalazimishwa kwa nini aliukataa. Kuna jambo moyoni mwake analijua ingawa hakusema hakubLiani nalo.kalazimishwa na kalazimishwa kuwakubali watu wa Kikwete wenye madhambi makubwa ambao inambidi awatumbue.kasogezew na kaambia wapokee hawa kwa nguvu. Tusiwe kama yuda iskarioti.alimbusu Yesu kuhusu akamatwe na akauawa. Hawa waliompeleka huyu kijana ni kama mayuda pia.badala ya kumhumu mtu jihukumu mwenyewe. Watu watakuwa hawana uhuru kuzungumza kwani jirani atawapeleka mahakamani. Hii ni dhambi kubwa.
ReplyDeleteSijui watakamata wangapi, wakati huyo mpuuzi hana heshima kwa raia wake. Ukweli uko palepale, atabaki kuwa Bwege, Fedhuli,Dictator,Mkurupukaji,Mropokoji, hana sifa ya uongozi. Screw you Ngosha!!!!!
ReplyDeleteAllah atuhifadhi ndugu zangu watanzania lkn kwa mpango huu hatuna salama
ReplyDeleteHapo big up brother au sister. Rais Magufuli hana shida hajawahi kumpeleka mtu mahakamani ila hawa polisi wanalilia vyeo. Na mwenye noah naye anataka ukuu wa wilaya ndio maana kampeleka huko. Kutukanwa unapotenda mema au mabaya hutakwepa kwa jamii kubwa kama hii. Najua na ninafaham Mhe. hawezi kumfunga mtu kwa kosa la kumtukana ila makabwela ndio wanaweza kufanya hivyo pole sana. Naunga mkono utendaji wa JPM.
ReplyDeleteKwa nini sasa asiwaambie Polisi wamtoe huyu. Na yule wa Songea watu walimchangia pesa atoke na bado anaandamwa. Atoe kauli kwa polisi wako chini yake waache kutumia nguvu kunyanyasa wananchi na vijana wa kesho. Polisi wasomeshwe na wafuate sheria. Vijana someni jiungeni polisi mkomeshe haya. Na Raisi atende haki kwa Watanzania wasinyanyasike.Udictator ndio huu.
DeleteNashangaa polisi wa Tanzania kumogopa magufuli kiasi
ReplyDeleteMagufuli hataki wanafiki
Fanya kazi tu usitake sifa Kamanda
Viongozi kutukanwa na vichaa it's normal
Umechemsha kwa hili Kamanda
Sijui watakamata wangapi, wakati huyo mpuuzi hana heshima kwa raia wake. Ukweli uko palepale, atabaki kuwa Bwege, Fedhuli,Dictator,Mkurupukaji,Mropokoji, hana sifa ya uongozi. Screw you Ngosha!!!!!
ReplyDeleteNawewe unafuatiliwa, ipo siku yako wutakutia mkononi, we jifanye mjanja tu .......kwanza nyinyi wote mnaotukana hamjampigia kura JPM, tukaneni mpaka mchoke, HAPA KAZI TU
Delete