Kikwete: Nashukuru Mungu Kwa Kuutua Mzigo Salama Huku Nikiiacha Nchi Ikiwa Salama Tulii Kabisa

MWENYEKITI Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt.Jakaya Kikwete amesema anashukuru Mungu Kwa kuutua mzigo salama huku akiicha nchi ikiwa salama tulii kabisa.

Amesema kuwa safari yake ya urais ilianzia Bagamoyo akitokea wilayani hapo ambapo baada ya hapo alikwenda Kibaha kutangaza nia ya kugombea urasi nakudai kuwa amejisikia furaha kurudi tena Bagamoyo akiwa salama.

Amesema wakati akielekea kutangaza nia ya kugombea urais alikuwa na mtoto wake Ridhiwani Kikwete ambapo yeye alikuwa anaandika na Ridhiwani anachapa kwenye Komputa.

Dkt.Kikwete aliyasema hayo jana wilayani Bagamoyo katika hafla ya kumkaribisha Nyumbani baada ya kuitumikia nchi Kwa miaka mingi, ambapo iliandaliwa na Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani.

Alisema anashukuru Kwa Mara nyingine kurudi mahala alipoanzia na kwamba amemaliza salama na ameacha nchi ikiwa salama na imetulia tulii kama Maji kwenye mtungi.

Akikumbuka mchakato wa mwaka jana wa kumpata Mgombea ulikuwa na mambo mengi lakini mambo yalikwenda salama na hakuna lililokuwa limeharibika .

"Ilikuwa Kazi kubwa si ndogo lakini hatimaye wa kavuka na wakaingia kwenye uchaguzi ambao ulikuwa na vurumai" alisema Dkt.Kikwete .

Aidha alisema kuwa hata hivyo katika uchaguzi huo kulikuwa hakuna mtu ambaye alipatwa na tukio la kumpiga mwezake hali ambayo iliwashangaza hata nchi jirani.

Alisema kuwa katika kipindi chake cha uongozi amefanya kazi kubwa ya kusukuma maendeleo ya wananchi Kwa mikoa yote,wilaya zote bila ubaguzi wowote ule huku akikiri kukabiliana na Changamoto ya kunyoshewa vidole hususani pale alipojaribu kupeleka maendeleo Wilayani Bagamoyo kanakamba wananchi wa Bagamoyo walikuwa hawana haki.

Aidha Dkt.Kikwete alisema kuna wakati alisimamisha fedha za ujenzi wa barabara hiyo na kupeleka fedha hizo kujenga barabara ya Geita, Sengerema,usagala ,na kulizuka na Maneno mengi dhidi yake na hadi kufikia wabunge kulumbana.

Alisema hata hivyo anashukuru kwamba amemaliza salama na Kwa bahati nzuri amepatikana rais ambaye ana ari kubwa ya kuwaletea maendelea watu huku akitaka watanzania kumuunga mkono.

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Usitutie kutapika ili husu nini kujenga bandari bagamoyo na tanga wala mtwara
    Nenda mwana kwenda

    ReplyDelete
  2. Hahahaha unabaki mtu kucheka tuu sina cha kuandika

    ReplyDelete
  3. Ridhiwani. Ndiye anayetajwa kila kona kwa ufisadi mkuu huku na kule. Ndiyo kakumbatiwa. Kuna Watoto wengi wa maskini wameporwa ardhi, Wamebomilewa nyumba, Madini hawayajui ya kupewa bila hata ya kutoa senti moja. Wamekufa bila dawa, chakula, au sababu wazazi wao wamekufa na serikali yako ilifumba jicho.Hawana baba wala mama wa kuwatetea, kuwafariji, kuwapa hata maji ya kunywa. Hata kijumba cha kukaa hawana. Hata chupi hawa watoto zinawashinda. Wazazi wao aliuawa, kutoweka, kupewa ulemavu. Zanzibar, Zanzibar, Zanzibar, Raisi wangu mstaafu, mbona unefumba macho. Nchi salama, au watu kama Tanzania ijulikanavyo duniani kama nchi salama, je ni kweli? Wanapigwa wengine hadharani kwa Kuwatetea wanyonge, Wanaachishwa kazi sababu hawakukubaliana na uongozi wako na kuitwa wasaliti, Bado mnawafuatilia na kutaka kuwakomoa. Maisha ya familia zao je mnanayajua, mna yajali.Watoto wao watashindwa kwenda shule na kupata elimu safi, wanahofia maisha ya Wazazi wao na yao hawayajui ya kesho. Je raisi wangu hii ndiyo salama.
    Hatuwezi wote kuwa Ridhiwani, lakini tunaomba haki, usawa, uhuru, elimu, uzima,tunaomba usawa wa kutumia mali za nchi hii kufuata sheria za nchi hii zilizowekwa tangu tupate uhuru kwa manufaa ya watu wa nchi hii.Vilema, yatima, maskini, vikongwe, wake kwa waume Raisi wangu mstaafu. Si kwa watoto wenu ambao wamepewa kila kitu ambacho wengi wao hata hawastahili. Leo mnaturudishia tena umeturudishia viongozi waliosaidia kuuza na kusafirisha meno ya Tembo uchina. Wapo huru. Wamebaki na vyeo umewateua tena kutetea maslahi ya Wachache.

    Je hii ni salama. Je hii ni sawa. ? makongoro marehemu mwimbaji mkuu wa CCM aliimba hii akauliza je ni sawa? Wote waliitikia si sawa. Imekuwaje leo Raisi wangu mstaafu? Maji yamemwagika kipindi cha miaka ishirini hasa hii kumi.Yatazoleka haya? Vijana wanaamka kisiasa wanafungwa midomo. Je hii ni Tanzania au Tanzayenu?
    Kama mmekosea, Jamani Tuambieni na tuanze mijadala safi kuisafisha , na kuijenga upya Tanzania yetu nchi tukufu ya Watanzania wote kwa usawa, haki, sheria bora na Katiba mpya inayokubalika na kuwatetea wote. AHSANENI.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mbona wewe 11.49 hapo juu baba yako ni fisadi kiwembe bwa.Machache na bado tunamvumilia!?

      Delete
  4. umeacha ufisadi uliokithiri katika maraisi wote,au kwako unaona sawa baba wa chalinze?

    ReplyDelete
  5. Pumzika salama salimini In Shaa Aalaha Mwenyezi Mungu atakulinda ulijitahidi kufanya kadri ulivyoweza

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad