Ripoti inaonyesha kuwa kinga dhidi ya Ukimwi haifanyi kazi kwa wasichana ukanda wa kusini mwa jangwa la Sahara huku wengi wakihitaji msaada wa kinga ili kuepuka maambukizi mapya.
Mkurugenzi mkuu wa UNAIDS,Michel Sidibe ametoa ripoti inayosema kuwa Kati ya asilimia 75 ya maambukizi mapya barani Afrika, asilimia 10 hadi 19 ni wasichana vigori.
Ripoti hiyo imetolewa siku chache kabla ya mkutano wa kimataifa kuhusu Ukimwi utakaofanyika mjini Durban nchini Afrika Kusini kaunzia Julai 18 hadi 22 mwaka huu.
Ripoti hiyo ni na mapendekezo kuhusu namna ya kusitisha maambukizo mapya na kufikia malengo ya 2020 kama ilivyoelezwa kwenye tamko la kisiasa la mwaka 2016 lililofikiwa mjini New York mwezi Juni
Kinga ya Ukimwi Haifanyi Kazi Kwa Wasichana
0
July 14, 2016
Tags