Kituo Cha Dk. Mwaka Chafutiwa Usajili, Wengine kusimamishwa miezi 6 na kupewa onyo kali


Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala nchini, limekifutia usajili wake wa kutoa huduma za kitabu, Kituo cha Tiba Asilia cha ForePlan Kliniki kilichopo Ilala Bungoni jijini Dar es salaam, kinachomilikiwa na Dkt. Juma Mwaka maarufu kama Dkt. Mwaka, kwa madai kuwa kimekiuka taratibu za kitabu za tiba mbadala.

Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa Baraza hilo, Dkt. Edmund Kayombo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, kwenye Ukumbi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Akizungumza jijini Dar es salaam leo katika Mkutano na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Baraza hilo, Dk. Edmund Kayombo amesema kuwa kufutiwa kibali cha Dk. Mwaka kunatokana na sababu nyingi ambazo amekuwa akikiuka licha ya kupewa maonyo na barua juu ya utoaji huduma zake.

Amesema sababu nyingine ni kuwa katika matangazo yake amesema anatoa tiba za kisasa wakati hiyo elimu hana ya kufanya huo.

Wengine waliofutiwa usajili ni Fadhaget Sanitarium kinachoendeshwa na Tabibu Fadhili Kabujanja pamoja na Mandai Herbal Clinic kinachoendeshwa na Tabibu Abdallah Mandai

Hata hivyo limetoa adhabu mbalimbali kwa kituo cha Aman Herbal Clinic kinachoendeshwa na Tabibu Esbon Baroshigwa, na Tabibu Castory Ndulu wa Kituo cha Ndulu Herbal Clinic wamepewa barua ya onyo.

Aidha wengine wamesimashwa kwa miezi sita ambao ni Tabibu John Lupimo wa Lupimo Suntarium Herbal Clinic pamoja na Tabibu Simon Rusigwa wa Sigwa Herbal Clinic.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwa kasi hii ya anko magu mjini pagumu siku hz wale wenye jeuri ya kuweka majina kwenye plate number zamagari jeuri kwishaaaa...wale wa jeuri ya pesa za unga sahv kimyaaaa wale wa jeuri za mishen town na kuuza vifaa vya wizi na magari ya wizi sahv kimyaaaaaa hahahh anko katushika pabaya mnoo sahv mwenye kazi ya halali ndo tajiri mjin maana tulikuwa hatuheshimiani kabisaa...kaza baba magu...dua zetu unazo...watakuchukia lakn watanyooka na hv huna ushkaji na mtu hahahhahahha kama naona mapedeshee walivyo na sura ndogo huko..waliko

    ReplyDelete
  2. its high time he goes to the medical school and becomes a real doctor ,

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad