Kutana na Mtandao Mpya wa Kijamii Kwa Ajili ya Kukuza Secta ya Utalii Tanzania 'EZYLINC '

Ezylinc ni mtandao mpya wa kijamii, ambapo watu binafsi na makampuni wanaweza kuweka
picha na kuandika makala kuhusu vivutio vya utalii vilivyopo nchini.

Mtu yeyote anaweza kujiunga na mtandao huu wa kijamii bure kabisa kwa kujisajili
www.ezylinc.com , baada ya hapo anaweza kuweza picha, kuandika makala kuhusu vivutio vya
utalii, kutengeneza magroup, kukutana na marafiki wengi zaidi kutoka sehemu mbalimbali
duniani na mengine mengi.

Ezylinc inaunganisha makundi mawili. Upande mmoja tuna watalii, na kwa upande mwingine
watu wanaofanya kazi zinazoendana na shughuli za kitalii.

Hapa Tanzania kama mfano, utalii ni sekta inayoliingizia taifa fedha nyingi za kigeni. Katika mwaka
2014 sekta ya utalii, imechangia asilimia 17 katika pato la taifa na kuchangia kwa asilimia 25 ya
mapato yote ya fedha za kigeni, ambapo bilioni 2 za Kimarekani zilipatikana.

Tanzania ni nchi yenye vivutio vingi vya utalii katika bara la Afrika. Kilimanjaro mlima mrefu kuliko
yote Africa, Visiwa vya Zanzibar, hifadhi za taifa za Serengeti na Ngorongoro, Tarangire, Ziwa
Manyara, Ruaha na Selous, ni mifano hai michache ya vivutio vinavyopatikana Tanzania.

Kwa kutumia mtandao huu mpya wa kijamii tunaweza kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini
kwetu kwa urahisi zaidi, na kupata watalii wengi zaidi.

Hii ni moja ya sababu kubwa kutengeneza mtandao mpya huu wa kijamii. Tunalenga kusaidia
ukuaji zaidi wa sekta ya utalii nchini, na hiyo itasaidia watu wengi zaidi kupata ajira katika shuguli
zinazoendana na sekta hii.

Karibu - Kujiunga Ezylinc, Ingia: www.ezylinc.com
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nawapongeza mliobuni wazo hili la kuanzisha mtandao huu. Huu ndiyo ubunifu chanya unaotakiwa wa kizalendo ambao utasaidia kuzalisha ajira kwa vijana wetu na kuliongezea taifa letu kipato. Ni ukweli usiopingika kwamba Shirika letu la Utalii bado liko nyuma saaaaaana katika suala hili la kutangaza vivutio vya utalii na kubuni mikakati shindanishi katika soko husika. Nilishtuka hivi majuzi kusikia kule kusini mwa ziwa Tanganyika mpakani na Zambia kuna maporomoko makubwa na mazuri ya mto Songwe na mabaki kibao ya zana walizotumia watu wa kale ambayo hayatangazwi hapa kwetu TZ! lakini Zambia sasa wanajitangazia kwamba yapo kwao. tujitangaze jamani hawo Kenya sasa tuwadhibiti walianza na Kilimanjaro sasa wamehamia Olduvai Gorge, Serengeti na Ngorongoro bila haya. Karibu wilaya zote zina vivutio kama kule wilayani Kondoa kuna Chemchem ya ajabu ya maji moto inayozalisha maji yanayotumiwa na mji mzima wa Kondoa enzi na dahali, daraja la mjerumani la kunesanesa. Michoro ya watu wa kale kwenye mapango ya mlima Tura na Kolo na mengine mengi tu. Huko Kyela na Rungwe nasikia kuna Kimondo kikubwa kilichoanguka kutoka angani na pia lipo 'Daraja la Mungu'.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad