LOWASSA Aitamani 2020, Awataka Vijana Kuanza Kujipanga Mbio za Urais 2020

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Democrasia na Maendeleo CHADEMA ambaye pia ni waziri mkuu mstaafu Mh. Edward Lowassa amelitaka baraza la vijana la CHADEMA Taifa kutokukubali kugawanywa katika misingi ya kisiasa na badala yake wajikite katika kukiimarisha chama hicho katika ngazi ya chini hasa vijijini.

Waziri huyo mkuu mstaafu ambaye pia ni mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA Taifa  Mh Edward Lowassa ametoa rai hiyo kwa vijana wakati wa ufunguzi wa mkutanao mkuu wa kamati tendaji ya BAVICHA Taifa na ambapo amehimiza umoja ndani ya baraza hilo na kuwataka kuelekeza nguvu zao mwaka 2020, huku pia akiendelea kusikitishwa na kauli tata za katazo la mikutano ya kisiasa.

John Mrema na Bw. Patrobas Katambi ambaye ni mwenyekiti wa baraza hilo pamoja na masuala mengine wamewataka vijana kuwa mstari wa mbele kuhakikisha demokrasia inapatikana huku pia adhima yao ya  kuelekea mjini dodoma wakisema iko pale pale.

Kikao hicho cha kamati kuu tendaji ya BAVICHA Taifa kilihudhuliwa na wajumbe kutoka mikoa yote Tanzania ambapo pia kinaratajia kutoka na azimio la njia mbadala ya kile inachokiita ni kwenda kulisaidia jeshi la polisi mkoani Dodoma.

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hapa kazi tu sio siasa au bla bla endelea kutamani tu. Tamaaa mbayaaa atii!!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nchi imeshapata tuliyekuwa tunaomba kila siku,sasa kuna haja gani ya kubahatisha kwa Lowasa tena?JPJM NI MPAKA 2025.GOD BLESS TANZANIA.

      Delete
  2. Nilikupenda,nakupenda ila kura yangu 2020 sikupi ng'o.
    Kitendo cha kususia bunge kinaniuma mpaka leo,mmetunyima haki tuliowachagua,mlitakiwa mpambane mpaka dakika ya mwisho kuliko kususa,mmetutia aibu sana.

    ReplyDelete
  3. We Babu Lowassa tumekuchoka hata muonekano wako na hivi vyombo vya habari, tatizo lako au lenu mlikuwa madarakani muda mrefu, lakini mlikuwa ni kampuni za mufilisi wa Taifa hili, alafu hamkuwa na maadili ya uongozi, na hata mikakati au mustakabali wa Taifa, kwa muda mrefu sana uliokuwepo kama kiongozi au viongozi, sasa mambo yanaenda vizuri Kabisa chin ya mpedwa Babab Magufuri, naye Wala si wa muda mrefu kama wewe. wewe Uanze tu, maanake tukiona sura yako, unatukumbusha Yale yalee, mmhhh ni kama kurudi nyuma baada ya kusonga mbeleee. Si urudi kijijini ulikokusema, kwamba utabolesha mifugo yako ya uchungajiiii,

    ReplyDelete
  4. INGAWAJE MIMI SIO MTZ LAKINI KWA KASI NA NAMNA KAZI YA MAGUFULI CHADEMA ONDOENI WAZO LA KUMUWEKA LOWASA TENA.

    ReplyDelete
  5. Daah,mkuu mimi nakumbuka safari ya matumaini tu,
    sijui itakuwa tena kama vile.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad