Mahafali ya KKKT Chuo Kikuu Muhimbili Yapigwa Marufuku Baada ya Wanafunzi Hao Kumwalika Lowassa Kuwa Mgeni Rasmi

Uongozi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) umezuia mahafali ya wanafunzi  waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT ) yaliyokuwa yamepangwa kufanyika jana mchana chuoni hapo jijini Dar es Salaam, ambapo Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa alikuwa amealikwa na wanafunzi kama mgeni rasmi.

Mahafali hayo yalizuiwa jana saa 6 mchana ikiwa ni saa mbili kabla ya muda kuanza

Tangazo lililobandikwa chuoni hapo na kushuhudiwa na wanahabari likiwa linamnukuu Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Apollinary Kamuhabwa liliwataka wanafunzi hao kutoweka mikusanyiko ya aina yoyote chuoni hapo.

Profesa Kamuhabwa kupitia tangazo hilo aliwaonya wanafunzi hao kutojihusisha na masuala ya siasa wawapo chuoni kama ilivyo kwa watumishi wa umma.

Jitihada za waandishi wa habari kuzungumza na uongozi wa chuo hicho ili kupata ufafanuzi ziligonga mwamba baada ya kuelezwa kuwa hawakualika mkutano na waandishi wa habari.

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Si waende kufanyia hayo mahafali yao huko Kanisani(KKKT)? mbona mnachokoza mambo wakati kila kitu kinaeleweka? hicho ni chuo mali ya serikali hakuna kufanya siasa hapo.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwani upinzani wanatoka nchi gani wasitumie mali za nchi yao?

      Delete
    2. Tatizo kubwa hapo haitakuwa shughuli iliyotajwa tu bali na mambo ya siasa ya uchochezi lazima yachomekewe.

      Delete
  2. Lowassa tishio la inchi!

    ReplyDelete
  3. hivi kumualika Lowasa kwenye mahafali ni siasa? Hii inatisha

    ReplyDelete
    Replies
    1. Haitishi bali ni kwa kuwa CHADEMA wanataka shari,wasituharibie nchi,wee mtu uko msibani lakini wanaingiza siasa sembuse huko kwenye mahafali.

      Delete
  4. How do we get freedom without being milled or bulldozed.It is scary.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad