Mahakamani Kisutu: Watatu Mikononi Mwa Polisi Kwa Kubeba Mabango ya Kumkashifu Mtukufu Rais Magufuli

Jana wafuasi wa UKAWA walitiwa mbaroni baada ya kutoke mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe wa kumkashifu Mtukufu Mkuu sana, Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Joseph Magufuli.

Baadhi ya Mabango yalikuwa yanasomeka...

Dikteta uchwara utashindwa
Dikteta uchwara nenda Burundi

Maoni Yangu;
Kuna msemo usemao Delegatus Non Potest Delegare wakimaanisha la kujitakia halina majuto. Hawa wafuasi naona wamejitakia au wametumwa na viongozi wao uchwara kubeba mabango ya kashfa kwa Rais. Mbowe alikuwepo mahakamani, kwanini yeye hakubeba bango la kashfa? Kwanini awatumie wafuasi wachache wasiojielewa?

Hivi nalo hili mtalalamika kuonewa?
Kwanini hamuheshimu Taasisi ya Urais?
Kwanini hamuheshimu Rais?

Mnataka nini hasa wana wa upinzani?

Tags

Post a Comment

15 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hapo ndipo wapinzani mnapochemka,na siku zinavyozidi kusonga ndio mnazidi kukosa sifa kwa sisi wananchi tuliokuwa myuma yenu.
    Uko Tanzania na unatetea watanzania sasa hayo ya burundi yanakujaje kwenye mabango?una uhakiki kuwa burundi kuna udikteta?kuonyesha kwamba chadema ni chama makini kweli kwa nini usimkemmee huyo aliyebeba bango la maneno ya dhihaka kabla ndipo uongee na waandishi wa habari?

    ReplyDelete
  2. Mimi ni mpinzani lakini kuna mambo mengine sikubaliani nayo kabisa, na kwa namna hii kuna kila sababu ya kutafakari kabla ya kutenda.JPJM ameshakuwa Mkuu wa nchi hata kama kuna kumpinga alichaguliwaje,lakini ameshaapishwa na dunia inamjua kwamba ndio rais wa TZ,unapomsemea maneno ya kejeli maana yake unamtukana rais,Mbowe ni kiongozi sasa kwa nini unawapanga wenye mabango mabovu na unapiga nao picha?Sikuelewi kiongozi.Badilikeni,siasa sio uadui.

    ReplyDelete
    Replies
    1. mnashangaza sana. hivi nini maana ya Demokrasia? demokrasia ni kuruhusu watu kutoa madukuduku yao. upinzani lazima uwepo ili nchi ikae vizuri. Nyie mnaishi dunia gani mbona watanzania hawana maarifa? nyie mnafikiri sifa lakini chama kimoja pekee katika nchi kikishapata nguvu kitafanya madudu wawezavyo. msifikiri wao ni wajinga kutaka kuua vyama vya upinzani. mtalia nyie msio na hekima wala kujua nini kinaendelea duniani. Nchi zote zenye maendeleo ya kweli zina vyama vya upinzani. nyie ndio nani hamtaki? mbona Republicans na Democrats wanabishana kila siku na bado nchi inaenda vizuri tu? tatizo viongozi wa kiafrika wanapenda kuabudiwa. no, wa kuabudiwa ni Mungu peke yake

      Delete
    2. anony wa 12.09pm fuatilia kwanza kinachoandikwa nasiyo kulopoka tu na kuandika off point/pointless

      Delete
    3. Huna hekima wala upeo wewe,hivi kumuita mtu dikteta wakati sio ndio demokrasia?au hujui maana ya dikteta?
      Fyuuuuuuuuuuuuuu,povu tu.

      Delete
  3. Mmmh,dikteta?dikteta asiyeua mbona poa tu.
    Nina imani na Magufuli kuliko maelezo,na kwamba huu ugumu wa maisha ni mapito ya muda mfupi,ninamuombea azidi kuipaisha Tanzania.Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  4. KELELE ZA CHURA HAZIMZUI NG'OMBE KUNYWA MAJI.
    WENYE MAPEMZI MEMA NA TANZANIA TUMUOMBEE MAGUFULI.

    ReplyDelete
  5. JPM tuma watu Zimbabwa wakakuambie ni vipi walisambaratisha Upinzani na hata wafadhili wa upinzani ambao ni UK US na EU,, Kanisa ambalo lilikuwa ndo njia ya kupitishia vyote lilifanyiwa nini??? Kumbuka Askofu mkuu wa Anglican nchini Zimbabwe yuko wapii??? Tupeni kazi na utaona viongozi wa Upinzani mtawaona wakicheza bao la kete masaa 24 na kujitoa kwenye siasa,,, mbona rahisi hasa kwa watanzania jamani!!!! Tumechoka na huu upuuzi wa upinzani usio na maadili ambao sera zao ni matusi yasiyo na msingi wakati dai lao ni moja tu BUNGE LIVE walipolikosa hilo basi ni matusi tuuu kila kukicha

    ReplyDelete
    Replies
    1. wewe ndio mjinga sana. Unataka Tanzania iwe kama zimbabwe kwa lipi jema walilo nalo sasa hivi? huo umaskini unaonuka mpaka chooni? huna hekima wala busara.

      Delete
    2. anony wa 12.05pm wewe ndo mjinga wa kwanza na mpumbavu, huo umasikini unaousema hata nchi za ulaya upo, jifunze kuandika sense, kwanza huna adabu mpaka kwa kizazi chako shenzi kabisa

      Delete
    3. JPJM alishasema atashirikiana na vyama pinzani katika kujenga nchi,lakini cha ajabu hata kabla ya bunge walikuwa wakipewa mialiko kwenye mambo ya maendeleo hawaendi,jiulize kwa nini,sasa hapo unadhani wapinzani wana nia njema na tanzania.HAPANA.

      Delete
  6. vijana tumekuwa mitaji kwa watu wenyewe pesa hasa kwa kukosa fikra yakinifu,tunakubali kutumikishwa kwa vitu vya kijinga hasa hawa wanaojiita wanasiasa,badara ya kusema tufanye kazitunalala tu huku tukitaka maisha mazuri mwisho wa siku tunatumiwa kama hawa ndugu zetu,ki ukweli kwa mtu mwenye akiri timamu hauwezi kubeba bango kama hilo kwa mh,raisi yatupasa kuheshimu srkl na tusikubali kutumikishwa mbona wao hawakubeba au ndo uwezo wetu mdogo kufikiri,tulikuwa tunalilia kiongozi mwenye kutoa kauli na kufuatilia mambo yanaendaje sasa mwenye kupiga vita rushwa,ufisadi,matumizi mabaya ya mali ya umma sasa tunafanya haya ni AIBU SANA kwa taifa letu,naumia kuona vijana wenzangu tunatumiwa kwa mambo yasiyo ya msingi,kwa namna hiyo UPINZANI HAWANA HOJA ZA MSINGI NA KAMA LENGO LAO NI KUTAKA KUIKOSOA SRKL kwa namna hiyo wajue wamekosa MWELEKEO cha msingi na ninawashauri washirikiane na Mh raisi ktk kuleta maendeleo nchini na taifa letu lisonge mbele pia vijana tusikubali kutumiwa kwa wenye mitaji ya kifedha,siasa kwa manufaa yao

    ReplyDelete
  7. Mbowe hawezi kuwazuia watu wake wajinga na wasiojitambua kwa sababu yeye ndiye alaiyeandika maneno hayo ya kumkashifu MHE, RAIS. Chadema obviously imekufa na wao wanajua na ndiyo wanaona sehemu ya kujirejesha kwenye siasa ni kuanzisha fujo na kuvunja sheria maksudi.Kwa serikali ya JPM,ni kufuata sheria, taratibu na kanuni na kuwabana pale wanapojivisha joho la Demokrasia kuvunja sheria. Tena wale ambao wamebeba mabango ya kashfa kwa JPM wafungwe miaka saba na faini ya shillingi milioni Ishirini na hakuna dhamana. Hawa wamisha kuwa wendawazimu usiwape kioo wajiangalie wanafikiria anayeonekana kwenye kioo hicho ni mtu mwingine na kuanza fujo au kutaka kupigana au kuzungumza na mtu huyo kumbe ni yeye mwenyewe.Poleni sana wapinzani ni wazi demokrsia na siasa kwenu ni mzigo usiobebeka na ni bora kutafuta kazi nyingine,hasa biashara na kuendsha kumbi za usiku na disco.

    ReplyDelete
  8. haowameandika dikteta lakini hawaja ainisha jina lolote

    ReplyDelete
  9. Hao wote wanaompinga muheshimiwa JPM walikuwa wanatunyonya,kutuibia huku tukiishi maisha ya dhiki mlo moja kwa siku kwa ugumu wa maisha huku vizazi vyao vikisoma shule za maana na kuishi kifahari sasa wanatapatapa.Yote yanamwisho hayo.JPM tupo pamoja kusafisha mafisadi.God bless our president.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad