Mastaa Wanaobadili Dini Kisa Ndoa Watumbuliwa


Baadhi ya wasanii wa filamu Bongo waliowahi kufanya uamuzi wa kubadili dini kutoka kwenye Ukristo kuingia kwenye Uislam ‘wametumbuliwa’ kufuatia mienendo yao isiyokubalika


Masupastaa hao wakiwemo Jacqueline Wolper, Rose Ndauka, Flora Mvungi, Aunt Ezekiel na Ester Kiama wametumbuliwa kutokana na kutoonesha jitihada zozote za kuijua vilivyo dini waliyoiendea.


Akizungumza na Ijumaa, hivi karibuni, Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Musa Salum alisema kuwa, kitendo cha mtu kubadili dini kisha kutoonesha utofauti hakuna maana na ni bora kubaki kwenye dini ya awali


“Kwanza wanaokosea ni wale wanaowasilimisha maana wakishawabadili dini hawafanyi jitihada za kuwatafutia watu wa kuwafundisha misingi ya Dini ya Kiislam, matokeo yake sasa unakuta mtu amebadili dini na kupewa jina la Kiislam lakini hafuati misingi ya dini.



“Lakini pili, hawa wanaobadili dini wenyewe hawaoneshi kutaka kujifunza, wanaridhika na ile hali ya kuambiwa wamesilimu na kupewa majina mazuri ya Kiislam lakini baada ya hapo wanabaki walewale,” alisema shehe huyo.

Wolper, Rose, Flora, Aunt na Ester ni kati ya wasanii wa Bongo waliosilimu huku baadhi yao wakifanya hivyo kufuata imani za wachumba zao ili waolewe lakini mpaka sasa hakuna aliyeonesha utimilifu wa kusilimu kwake, badala yake baadhi yao wameendelea na mifumo yao ya maisha kama walivyokuwa wakiishi walipokuwa Wakristo.

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. ulishasema wasanii unategemea nini?

    ReplyDelete
  2. maneno ya Mr. Kasari ni kweli kabisa hasa kwa hawa wanawake wanaowataka wanaume wa kiisalan kwa mfano wolper hii mara ya pili aunty ezikel pia na bado yupo kwenye ndoa na sasa kapata bwana na kazaa nae isutoshe mavazi wanaova ni kinyume anausilimishwa kwanza lazima apelekwe kupata elimu ajue sheria na afuate sio unakurupuka unasilinu na unafanya yako musicheze na dini

    ReplyDelete
    Replies
    1. Anon si kwamba wanaowataka wanaume wa Imani hii au ile. Sisi sote ni wamoja na tunaishi Katika jamii moja, kompenda Huyu au yule Sio mbaya na kupenda ni hulka ya binadam. Na maswala dini ni ya Imani iliyojenga katika miyoyo na mienendo yetu ya Kila siku kwa maisha ya mwanadam, na dini Sio kikwazo cha kututenganisha, eti uwezi kuolewa na Huyu au yule umpendae imani ni mapokeo. Na kwa jamii yetu ya Kiafrika tumezipokea toka kwa wenzetu, na yote ni katika kumuweka mwanadam ajitambue kwa matendo yake na angalau kumjua muumba wa vitu vyote ya kwamba tumeumbwa, sio mpaka awe baba na mama yako tu ndio unaowatambua na angalau kutendeana yaliyo mema kuonyesha hofu juu ya muumba. Kwa hiyo kubadilisha ili kufwata mume ni kwa sababu ya upendo na kubadilili si kosa bado linabaki paleple Iman. Kwani dini ikisha mkolea inamaana imani imekolea na kujengeka aswa ni kwa mwanadamu yeyote yule, ndio maana tunasema imani ni kitu kimjengacho mtu na upendo ni kitu kitokacho moyoni

      Delete
  3. Wanajua maisha Ni hapa Tu duniani,wanajisahau Sana Kuna maisha tena baada ya haya.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad