Mbunge Peter Msigwa Atuma Barua kwa Spika Ndugai


Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa (CHADEMA) amesema amewasilisha barua kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai akitaka Naibu Spika aondolewe madarakani kwa kukiuka kanuni za uendeshaji Bunge.

Akizungumza na waandishi wa habari Msigwa amesema kwamba muswada wa fedha uliopitishwa na Bungen lililomalizika ulipitishwa kinyume na taratibu.

''Muswada wa fedha wa mwaka 2016 wenye namba 9 ulichapwa tarehe tarehe 03 Juni 2016 na kusomwa bungeni kwa mara ya kwanza na kwa utaratibu wa bunge ukaenda kufanyiwa kazi na kamati ya bajeti na katika katika majadiliano na wadau ikaonekana muswada huo ulihitaji marekebisho makubwa hivyo serikali ilitakiwa kuleta jedwali la marekebisho jambo ambalo halikufuatwa''- Amesema Msigwa.

Msigwa ameongeza kuwa ''Naibu Spika amekiuka kanuni na namna muswada huu ulivyopitishwa hata wabunge wa CCM wengi hawakukubaliana nao ila yeye akaupitisha''
''Kwa mantiki hii nimemwandikia barua Spika wa Bunge kwa kutaka kumuondoa Naibu Spika Tulia Ackson Mwasasu kwa kushindwa kusimamia kanuni za bunge wakati wa kupitisha sheria ya fedha ya mwaka 2016'' amesema Msigwa.

Wabunge wa kambi ya upinzania katika bunge la 11 mkutano wa 3 uliomalizika walisusia vikao kwa zaidi ya wiki 3 wakitoka nje baada ya kudai kwamba Naibu Spika Dkt. Tulia Mwansasu anaendesha Bunge isivyo.

Hata hivyo Naibu Spika alisikika akisema anaendesha Bunge hilo kwa mujibu wa kanuni na kama wabunge hao wanatatizo na uendeshaji wake wa bunge watumie kanuni na si kususia vikao vya bunge.
Tags

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hawa tunawajua na Huyu tunamjua! wangelikaa na kuwajibika hiyo nafasi walikuwa nayo na wanayo.. Kwa hivyo hayo madai batili hayana mshiko.. Kama ni muswada ulitengwa na wakaingia mitini/Vibarazani na kutochangia na bunge letu tukufu uwepo usiwepo wachapakazi na wa jibikaji wapo kazini na si hii tu na mengine yataletwa na tutajadili na ikibidi kupitishwa Hatuto sita wala kungoja wavivu na wazembe toka vibarazani... mpo vijana wangu.. kumbukeni huu ni wakati wa kumtumikia Mtanzania na kumletea Maendeleo..Sio Vioja na sarakasi.. tumelikataa Hilo posho pia hakuna kila ukiingia mitini..mtaenda fesibuku ssssssanaaaa lakini tumewastukia Wapotofu nyinyi..HAPA KAZI TU..UKIWEZA KUJITOA KATIKA KUBURUZWA NA KUTUMIWA KARIBU UJENGE TAIFA...

    ReplyDelete
  2. Hawa tunawajua na Huyu tunamjua! wangelikaa na kuwajibika hiyo nafasi walikuwa nayo na wanayo.. Kwa hivyo hayo madai batili hayana mshiko.. Kama ni muswada ulitengwa na wakaingia mitini/Vibarazani na kutochangia na bunge letu tukufu uwepo usiwepo wachapakazi na wa jibikaji wapo kazini na si hii tu na mengine yataletwa na tutajadili na ikibidi kupitishwa Hatuto sita wala kungoja wavivu na wazembe toka vibarazani... mpo vijana wangu.. kumbukeni huu ni wakati wa kumtumikia Mtanzania na kumletea Maendeleo..Sio Vioja na sarakasi.. tumelikataa Hilo posho pia hakuna kila ukiingia mitini..mtaenda fesibuku ssssssanaaaa lakini tumewastukia Wapotofu nyinyi..HAPA KAZI TU..UKIWEZA KUJITOA KATIKA KUBURUZWA NA KUTUMIWA KARIBU UJENGE TAIFA...

    ReplyDelete
    Replies
    1. Unadhani ni sababu zip zilizopelekea hayo??

      Delete
    2. Unafikiri kwa nini waliamua 'hivyo??'

      Delete
  3. We anonymous wa hapo juu. Niliomba endeleza elimu yako kabla u
    Ya kutoa hoja yako. Angalia maslahi yako, ya Taifa n.a. kizazi kijacho. Hawa wanaotoka nje sababu wengi wapinzani wenye juzi n.a. hii kazi naibu spika kawatoa nje. Kabwe. Mboye, mbunge wa Arusha, Mrema, Tunfu lisu. Hawa nfio vijembe vya hii kazi. Mbona hamfikiri mbali.
    Mnafunga maskini n.a. macho anapowaadhibu wenye uwezo sababu ans dhaifu. Mbona nyinyi vipofu wa akili. Elimu, ni ufunguo wa maids watanzania wenzangu. Mmezoea kipokea amri n.a. kulaza
    Akili n.a. kulalamika utu.

    ReplyDelete
  4. We anonymous wa hapo juu. Niliomba endeleza elimu yako kabla u
    Ya kutoa hoja yako. Angalia maslahi yako, ya Taifa n.a. kizazi kijacho. Hawa wanaotoka nje sababu wengi wapinzani wenye juzi n.a. hii kazi naibu spika kawatoa nje. Kabwe. Mboye, mbunge wa Arusha, Mrema, Tunfu lisu. Hawa nfio vijembe vya hii kazi. Mbona hamfikiri mbali.
    Mnafunga maskini n.a. macho anapowaadhibu wenye uwezo sababu ans dhaifu. Mbona nyinyi vipofu wa akili. Elimu, ni ufunguo wa maids watanzania wenzangu. Mmezoea kipokea amri n.a. kulaza
    Akili n.a. kulalamika utu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nyinyi mbi mguu mzungu WA. Reli mjiite vijrmbe..kweli nchi Itakuwa imekosa Wazalendo..hai wote Na wenzi Wao Ni wanasarakasi Na watovu wa nidhamu..Na wakosa mwelekeo..saba u Yao nainua Na uchu Wao tunaufahamu Na elimu Yao tunaijua Na upotoshaji Wao pia tunauelewa..nia zao pia tunazielewa Na malengo Yao tunayajua ..ila mbinu walizo Na wanazo zitumia wameumbuka.

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad