Meya Wa Jiji:
Yafuatayo Ni muhimu Kwa wakaaz wa Jiji la Dar kufahamu kama haki yao ya msingi kabla ya utekelezwaji wa amri ya Mh Mkuu wa mkoa wa Dar wa kufanya msako kwenye makazi na nyumba zao.
Moja: Kwanza zoezi hili ni BATILI na haliwezi kutekelezeka kwenye Halmashauri zetu za Jiji la Dar es Salaam
Pili: Nawaomba sasa nielezee sababu ambazo nasema agizo hilo na zoezi hilo litakuwa BATILI :
A. Sheria ya makosa ya Jinai Inaelezea utaratibu wa kukaguliwa nyumbani kama search warrant ambayo inatolewa Na Mahakama au polisi, Na ambayo Inaelezea wanatafuta nini
B. Sheria hiyo pia inamtaka mwananchi kuwakagua maafisa wa Mahakama Na Polisi watakaofika Nyumbani kwake ili wasiweze kumpandikishia ushahidi wa uongo
C. Kamwe popote duniani Kibali cha wananchi kukaguliwa majumbani hakiwezi kutolewa Na Viongozi wa kisiasa.
D. Kwa maagizo hayo inasemekana wananchi watawekwa ndani Kwa kukataa kutii agizo hilo, hakuna sheria Tanzania inayoruhusu Mwananchi kuwekwa ndani kwa sababu za hovyo Kama hizo.
Naomba nimalizie Kwa kusema wananchi wote wa Jiji la Dar wawe na Amani kabisa na wajue haki zao na wajue kuzitetea, sisi viongozi wao tupo imara kusimamia haki zao na maendeleo ya Jiji la Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla.
Issaya Mwita Charles
Mstahiki Meya Jiji la Dar es Salaam
Asante baba maana kuna mijitu inapenda sifa ni kama imelewa uongozi mixxxeeewww
ReplyDeleteMESSAGE WELL SENT AND WELL RECEIVED. TRUE DEMOCRACY, HAKI SAWA KWA WOTE ! SWALI KWA MKUU WA MKOA : ZOEZI LILILENGA WANA DAR ES SALAAM WOTE AU NI BAADHI YA MAENEO, HASA YETU YA WANYONGE USWAZI ?
ReplyDeleteMESSAGE WELL SENT AND WELL RECEIVED. TRUE DEMOCRACY, HAKI SAWA KWA WOTE ! SWALI KWA MKUU WA MKOA : ZOEZI LILILENGA WANA DAR ES SALAAM WOTE AU NI BAADHI YA MAENEO, HASA YETU YA WANYONGE USWAZI ?
ReplyDeletekwanini mnahofu ya kukaguliwa, huyu meya wa jiji uwezo wake mdogo sanaaaaaaa
ReplyDeleteUkishakaguliwa ili iweje...hakuna mwenye hofu...kuna mambo mengi ya kufanya zaidi ya hilo kama wanapita kutambua wakazi wa maeneo sawa lakn sio kupita kukamata watu wasio na kazi...ukishamkamata utaenda kumpatia kazi...wakati mwingine upuuzi tuweke pembeni tufanye yenye maana kama huna la kusema si lazima uongee kila siku...kwan ni lazma uonekane kwenye vyombo vya habari kila siku unatoa matamko...kukaa kimya pia ni utendaji...
ReplyDelete