Meya wa Kinondoni Atumbua Majipu Kwa Kufuata Taratibu Sio Misifa Kama Wale

Baraza la madiwani chini ya meya wa manispaa ya Kinondoni Jacob Steven limewachukulia hatua watumishi 18 waliokuwa na tuhuma mbalimbali, watumishi 9 wa uhandisi, 8 afya na 1 wa utumishi fedha na biashara,

Watumishi wa 4 afya wamefukuzwa kazi kwa utoro na rushwa, watumishi 3 uhandisi wamekutwa na hatia kwa kushushwa vyeo na madaraja na mtumishi wa fedha na biashara amepewa onyo kali
uamuzi kwa wahandisi umetokana na wao kushindwa kutumia taaluma zao vizuri kwenye ujenzi wa barabara.
watumishai hao walichukuliwa hatua baada ya kufunguliwa mashtaka, kufanyiwa uchunguzi wa tuhuma zao na wao kupewa muda wa kujitetea.

Baraza la madiwani limewapandisha vyeo watumishi 372, kuwabadilisha vyeo watumishi 9, na kuwathibitisha kazini watumishi 206 ambao walimaliza vipindi vya majaribio na kuonekana kuwa wanafaa kuwa watumishi wa umma

Nawapa hongera kwa kufanya kazi hii kwa weledi na sio kwa show off, wanaofanya kazi kwa show off ili kuonekana wanafanya kazi na wanapenda haki kumbe wana sura mbili wangeiga mfano huu

VIDEO:

Tags

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wewe mwandishi nae mnafki,kina nani wana sifa,fuata maadili ya Kazi yako acha umbea

    ReplyDelete
  2. yaani inaonesha jinsi gani we mwandishi hujaiva katika maadili ya uandishi, nenda shule tena. maana unaonesha umeegemea upande vidole viwili. sio inshu kasomeeeeeeeeee.

    ReplyDelete
  3. ovyoooooo sifa unazijua au unazisikia halafu utajiita mwandishi. nenda shule tena kibaraka wewe

    ReplyDelete
  4. HONGERA SANA MEYA!!!!

    ReplyDelete
  5. Wanajulikana wauza sura na watoa matamko kila siku asubuhiii hahhahaahha...li mtu linazungumza hovyo tu halijui hata mipaka ya kazi yake..mfyuuu

    ReplyDelete
  6. Kwani uwongo huyo mkuu wa mkoa kila siku nimetoa tamko hata mrejesho hatuoni

    ReplyDelete
  7. Mbona wanajulikana wanaofanya maamuzi kwa kukurupuka mara msako wa nyumba kwa nyumba kwa wasio na kazi,mara vilainishi yaani ni upepo tu

    ReplyDelete
  8. Tumbadilishe jina tumwite mista makonda misifa

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad