Mheshimiwa Rais, labda hili litakuwa gumu kidogo kwa wewe kuligundua maana viongozi wote wanapopita pale uwanjani huwa hawatumii njia na process hii ambayo sisi watu wa kawaida na wageni wanaotoka nje huwa wanaitumia katika kupata viza (tourist visa) ya kuingia nchini.
Pale kuna uozo mkubwa sana na si hilo tu basi upoteaji mkubwa wa fedha za serikali ambazo nadhani huwa zinaingia mifukoni mwa baadhi ya wafanyakazi na viongozi wao, ni mtandao ambao upo kwa muda mrefu tu. Ni usumbufu kwelikweli usiokuwa na sababu yoyote.
Sasa ninaelezea kwa kirefu:
Wageni wengi wanaokuja Tanzania na kuchukulia visa zao pale aiport huwa wanatozwa dola za kimarekani 50 ($50.00 Usd) na huwa hawakubali aina nyingine yoyote ya pesa isipokuwa dola za kimarekani tu. (hilo ni tatizo namba 1).
Wageni wanapofika basi kuna mtu (sijui ni nani na anatoka department gani) husimama pale na kukusanya passport zote na hizo dola 50 (kila passport huwekwa dola 50 ndani yake) huyo mtu huzikusanya bila hata ya kutoa risiti yoyote,(na kuwaambia msubiri) na kuenda nazo kusikojulikana (labda ni ofisini kwao) kwa ajili ya kuweka hizo viza, hapo sasa ndiyo kuna tatizo kubwa sana, Mtasubiri si chini ya saa moja ndipo mtarudishiwa passport zenu na viza tayari zimo ndani, akifika huyu mtu anaanza kuita majina na kukukabidhi passport zenu ili sasa muelekee uhamiaji kwa ajili ya kupata entry ya kuingia, wakati huo sasa wale wenzenu wote mliokuja nao wameshamaliza kupita kwa watu wa forodha na wako nje tayari.
Nimesikia kwa sasa hivi huyo mtu wa kukusanya hizo passport hayupo ila walichofanya ni kuweka kijiofisi kidogo ambacho hufanya hivyo hivyo, unafika pale kwenye hicho kijiofisi na kumpa passport na dola 50 (hawataki aina nyingine yoyote ya fedha) na HUPEWI risiti yoyote, halafu unaambiwa usubiri, baadaye anakuja mtu kuzikusanya passport zote hizo anaenda nazo ndani huko, hapo bado tena mtasubiri siyo chini ya saa moja au mawili ndiyo mrudishiwe hizo passport. Mimi nilishuhudia wageni wenye asili ya kizungu wakilalamika sana pale airport kuhusu huo usumbufu.
Sasa mimi maswali yangu ni kwa nini wanapenda kuwafanyia watu huu usumbufu? na hapo ni dhahiri kuwa kuna pesa nyingi tu ambayo badala ya kwenda serikalini basi huingia mifukono mwa watu.
Sasa Mheshimiwa Rais kama tuko kwenye kuitengeneza Tanzania hii kuwa nzuri, bora na ya uwajibikaji, kwa nini basi usisafishe na kulitatua tatizo hili? Mimi naamini kabisa kuwa wageni wengi wanaokuja TZ wakishapata usumbufu huu basi huwa hawarudi tena na badala yake wanakwenda nchi jirani.
Nini cha kufanya:
Nimetembelea nchi nyingi ambazo hutoa viza palepale airport (visa on arrival) na hukuti matatizo kama haya kwa sababu hakuna wizi.
Nchi 1: Hapa ukifika tu utakuta kuna ofisi, unaenda dirishani unampa passport yako na pesa au bank card (pesa ya kigeni yoyote inayotambulika, zote zimeorodheshwa pale), palepale anakubandikia visa (sticker) na unaelekea kwa uhamiaji. Kitendo hicho hakichukui hata dakika 5.
Nchi 2: Hawa hawataki fedha taslimu kabisa, ni bank card tu, ukifika tu unaenda kwa uhamiaji moja kwa moja, pale unafanya malipo kwa bank card yako, unapata risiti na anakugongea viza (mtu huyohuyo mmoja), kwa hiyo yeye hakamati fedha taslimu kabisa. Hapa sasa tunaweza kusema kwa wale wasio na card je? Jibu ni hivi, kwanza watu wengi wanaoomba viza hapo airport ni wageni na ndiyo maana wanaomba hizo viza, kwa asilimia kubwa ya hao watu wanazo kadi, na pili unaweza kununua Prepaid visa/mastercard, kwa wale wanaoishi ughaibuni watanielewa, kupata bank card huko ughaibunu siyo big issue.
Nchi 3: Hawa sasa ukifika unaenda dirishani kulipa kwa bank card au fedha taslimu, halafu anakupa risiti unaenda nayo kwa uhamiaji na passport yako na uhamiaji anakupigia entry visa kwenye passport yako na kwenye ile risiti, hapo huchukui hata dakika kumi.
Sasa mimi sisemi tuige hayo hapo juu (lakini kama ni mazuri kwa nini tusiige?) lakini tukichukua yote hayo na kuyachanganua vizuri basi tunaweza kutengeneza mfumo wetu wenyewe ambao hautampa mgeni usumbufu hapo airport. Pili ningependa pia kuiomba serikali hizi balozi zake ziwe zinajaribu kutoa visa kwa waombaji wake kwa haraka kidogo ili kuondoa nenda rudi nyingi.
Mimi naamani kabisa kuwa hilo tatizo linaweza kutatulika na mtiririko wa wageni unaweza kuongezeka, maana wenzetu wageni huwa hawapendi usumbufu, kwanza huwa wanakuja kutembea na hivyo huwa hawapendi kupata bugudha kama hizo hasa ukizingatia kuwa Airport ndiyo kioo cha nchi, maana ya kwamba mgeni akiona mwenendo wa pale airport (airport yoyote duniani) basi tayari inampa taswira ya nchi hiyo ilivyo.
Kwa hiyo Naomba Mheshimiwa Rais na waziri husika mlifumbulie macho suala hili, Fedha za serikali pale airport bado zinaliwa na wajanja.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu mbariki JPM
By Pepe17/JF
Mbona hutaji baada ya kurudishiwa passport huwa kuna maandishi ndani ya hiyo passport na muhuri wa uhamiaji kuashiria hizo dola 50 zimelipwa? Msitake kupotosha watu
ReplyDeleteRisiti huwa zinatolewa, sioni point yeyote ya huyu mwandishi..
ReplyDeleteWWEEE KAA KIMYA KUNA MADUDUD MENGISAAAANA PALE JULIUS K.NYERERE AIRPORT.WIZI WAKUPITLIZA...NAMAJIPU MENGI KILA DEPARTMENT MULE UWANJANI...
ReplyDeleteHii Ni observation yake. Na Mimi ntalifatilia kuhakiku kinacho zungumzwa..mpaka turishike..Maoni myatie Na sisi tupo Ili kurekebisha Na kubotesha..Mchango Ni nzuri Na mingine yeyite ambayoitasadiaa katila kuliimgizia pato nchi mnakatibishwa kuyaleta
ReplyDeleteMwandishi yuko sawa kabisa, mimi nimesafiri kwa Tanzania zaidi ya mara 8 na only mara moja nimepata kwasababu niliomba visa uko mtu kenda migration nakulipia uko, lkn kila siku ni mambo yale yale, sisi kufika mbona bado
ReplyDeleteMimi nimepita juzi hapo walichukua pasport yangu nikiwa mtu wa kwanza lakini cha hajabu nilirudishiwa hiyo pasport baada ya saa moja mpaka nika lalamika. Jamani kweli pana usumbufu mkubwa mno na cha hajabu wako wafanyakazi zaidi ya watu 20 pale lakini wanacho kifanya kweli sijui nini hina bidi wausika walifanyie kazi jamani ni usumbufu mkubwa sana hasa kwa siye tunao omba visa ya kuingia nchini tunateswa sana mpaka unajuta. No no no jamani tafuteni nini cha kufanya hili tukifika tusiwe tuna kaa mda wote huo.
ReplyDeleteKwakweli wanatutesa sana wageni jamani yaani huwa najiuliza kila siku kuna nini pale kinacho fanya watu wacheleweshewe visa zao nakusubili zaidi ya saa 1 nini hiki jamani! Mheshimiwa raisi hebu taribu kufatilia kuna nini nyuma ya pazia na ukizingati wamewajaza sana watu lakini utendaji wa kazi kwakweli ni %
ReplyDeletejamani ni kweli tupu, hata kurasini majanga tupu unaangaishwa mwezi.mpk utoe chchte utaonewa
ReplyDelete