Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Bw. Mkono amesema kuwa ulipaji wa kodi si kwa ajili ya wafanyabishara pekee, bali ni wajibu wa kila Mtanzania wakiwemo viongozi wa Serikali na kuongeza kuwa kitendo cha TRA kufunga Ofisi yake inayotumika kwa shughuli za uwakili ilikuwa sahihi kwani walitimiza wajibu wao kwa ajili ya kuboresha uchumi wa taifa.
Kampuni ya Nimrold Mkono inayojishughulisha na masuala ya Uwakili ilifungwa kwa kudaiwa Kodi ya Shilingi Bilioni Moja lakini hata hivyo Ofisi tayari imefunguliwa na kuendelea na shughuli zake.