Mlinzi Adaiwa Kujinyonga kwa Kuambukizwa VVU

Mlinzi wa  Kampuni ya  Ulinzi ya Imara , Samwel Alcado (39) amekutwa akiwa amejinyonga ndani ya chumba chake kutokana na kile kinachodaiwa ni kugundulika kuwa ana virusi vya Ukimwi (VVU).
Mlinzi huyo ambaye ni mkazi wa mtaa wa Mji wa Zamani Manispaa ya Mpanda amejinyonga kwa kutumia shati lake.
Mwenyekiti wa mtaa huo, Margret John amesema tukio hilo  limetokea  leo  majira  saa kumi na moja alfajiri ndani ya   chumba alichokuwa  akiishi   Alcado.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Damas Nyanda amethibitisha kutokea kwa kifo hicho akisema uchunguzi zaidi unaendelea kufanyika ili kubaini ukweli halisi wa tukio hilo.

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. kwa nini alijinyonga jamani wakati dawa za kurefusha maisha zipo angeweza kuishi maisha yake yote na dawa

    ReplyDelete
  2. MJINGA SANA HUYU. HIVI ANAYEUMWA KISUKARI NA UKIMWI NANI MGONJWA HASA???? UKIMWI UNAKULA KILA KITU NA MADAWA YA KUREFU MAISHA YAPO JE KISURARI?? HULI BAADHI YA VYAKULA, INAUA MACHO, VIDONDA HAVIPONI,UNAWEZA KUKATWA BAADHI YA VIUNGO AMBAVYO VIDONDA HAVIPONI. SASA HAPO NANI WA KUJINYONGA??????

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad