Msajili wa Vyama vya Siasa Alaani Tamko la CHADEMA

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi amelaani vikali  tamko la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) lililotolewa jana tarehe 27 Julai, 2016 kupitia vyombo vya habari, kuhusu hali ya demokrasia ya vyama vingi hapa nchini la kuazimia kufanya mikutano na maandamano nchi nzima akidai kuwa tamko hilo ni la kichochezi lililolenga kuleta uvunjifu wa Amani.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha Ofisi ya Msajili wa Vya Siasa na kusainiwa na Jaji Francis Mutungi imebainisha kuwa tamko hilo linaenda kinyume na Sheria ya Vyama vya Siasa namba 5 ya mwaka 1992 kifungu 9 (2) (c) inayokataza chama cha siasa kutumia au kuhamasisha matumizi ya nguvu au vurugu kama njia ya kufikia malengo yake ya kisiasa.

“Nimepokea kwa masikitiko tamko la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) lililotolewa jana tarehe 27 Julai, 2016 kupitia vyombo vya habari, kuhusu hali ya demokrasia ya vyama vingi hapa nchini. Tamko hilo limejaa lugha ya uchochezi, kashfa, kuudhi na lenye kuhamasisha uvunjifu wa amani. Ili kuepuka kurejea tamko lote, nimeona ni vyema nitoe mfano wa maneno yafuatayo yaliyosemwa, ambayo yanakiuka Sheria ya Vyama vya Siasa”. Ilisema taarifa hiyo.

Aidha, taarifa hiyo iliongeza kuwa kifungu cha 9(2) (f) kinakataza chama cha siasa kuruhusu viongozi au wanachama wake kutumia lugha ya matusi, kashfa na uchochezi ambayo inaweza kusababisha au ikapelekea kutokea uvunjifu wa amani. Vile vile kanuni za Maadili ya Vyama vya Siasa, Tangazo la Serikali namba 215 la mwaka 2017, zinakataza chama cha siasa kutumia lugha za matusi, kashfa, uongo na uchochezi.

Nakuongeza kuwa kanuni ya 5(1) (d) inakitaka kila chama cha siasa kutotoa maneno yoyote au maandishi ambayo ni uongo. Kuhusu mtu yoyote au chama cha siasa chochote.

Katika taarifa yake Jaji Mutungi amesema kutokana na Kanuni hizo tamko la CHADEMA ni ukiukwaji wa Sheria ya Vyama vya Siasa.

Aidha, hii siyo mara ya kwanza kwa CHADEMA kutumia lugha za namna hii za kuhamasisha uvunjifu wa amani (civil disorder).

Natumia fursa hii kukemea tamko hilo hadharani, kwa mujibu wa kanuni ya 6(2) ya Kanuni za Maadili ya Vyama vya Siasa. Pia nawaasa CHADEMA wasiendeleze tabia hii.

Jaji Mutungi ametoa rai kwa  Viongozi wa Vyama vya Siasa  waonyeshe ukomavu katika medani za Siasa badala ya kujikita katika vitendo, kauli au matamshi yenye mlengo wa kusababisha uchochezi au kufarakanisha Umma na Serikali yao.

Katika tamko lao CHADEMA wameitangaza siku ya tarehe mosi Septemba kama ni siku maalum kwao kufanya mikutano nchi nzima ikiwamo maandamano ambapo ngazi zote za chama kuanzia ngazi ya msingi hadi Taifa zitahusika.
Tags

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. lugha ya uchochezi!!!????

    ReplyDelete
  2. Nimesikiliza Kauli mbalimbali kutoka mkutano mkuu wa kumkabidhi Raisi Magufuli uenyekiti. Kashfa nyingi sana zimetolewa kuwalenga vyama vya upinzani na viongozi waliopita mmoja wao Waziri mstaafu Lowasa na Sumaye. Lakini Jaji husemi lolote. Hizo ni Kashfa za moja kwa moja.
    Nilimsikia Mkuu wa Polisi akisema hajakataza Mikutano ya hadhara. Lakini ni CCM tu inayofanya mikutano hiyo ingawa inatumia maneno ya chuki yenye kuhatarisha imani kati ya Vyama lakini hata mara moja haijawa na kosa lolote. Makosa yanaonekana kwa Chadema na Upinzani tu, je hiki hakileti chuki nchini na ndicho chanzo cha uhasama?
    Tunazungumzia sheria na vipande vya sheria hii kwa kila mtu anayefuatilia sheria hizi na zinavyotumika tofauti kati ya chama na vyama vingine hii ni Hatari kubwa nchini kiusalama. Kinachonishangaza, Ni kweli viongozi wote na wafuasi wa CCM wanaunga hili na hakuna hata mmoja anayeona uhalalia wa chama kimoja kuwa na msimamo tofauti kabisa na vyama vingine vyote? Je ni kweli Wanachama wote wa CCM wanakubakiana na hili? Hawaoni hata mara moja kwamba CCM inaendesha nchi kama ni chama pekee na mfumo ni ule ule kabla ya kuundwa vyama vya upinzani? Sasa kwa nini mmeiingiza nchi kwenye mfumo wa vyama vingi lakini mnakataa kabisa kuona hili? Kwa nini msikatae kabisa mfumo wa demokrasia na wa vyama vingi nchini. Sheria zote zinazotumika ni mfumo wa zamani. Na mfumo wa zamani ni CCM mpigie ndio au hapana. Picha ni moja tu hakuna picha ya mtu mwingine. Inamaana mtu mwingine haonekani kabisa. Mwekeni kikapuni. Bado tunaendelea na mfumo uleule kwa nini? Ni Amri tu fanya hiki au nitakuchapa.Hata mtoto hatumlei namna hii.Mtoto atakuuliza nimekosa nini unanichapa? nimefanya nini? Ukiuliza pia ni kosa. Haya basi.Ni hatari kubwa huku tuendako na hapa tulipo.

    ReplyDelete
  3. Hizi Sheria Vipi?
    Sijaona uchochezi wowote hapa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kama hutaki kuona hutaona. Sababu wewe pia ni mwana CCm na mtinfo na fikra zenu zote sawa. Nenda kwenye nchi zenye demokrasia uone faida za kuzungumza bila woga ndizo zinazoleta maendeleo . Na si unyanyasaji na kuwachunga watu kama hawana fikra huru na upeo .ni watu duni tu watachukua uamuzi na watu waoga.

      Delete
  4. bwabwa la ccm
    fyuuuuu
    Kuchu utamjuwa tu

    ReplyDelete
    Replies
    1. nafikiri wewe ndo bwabwa la lowasa na sumaye

      Delete
  5. Naona msajili anaendelea kufanya kazi ya ccm! Mmezuia vyama kufanya mikutano huku ccm wakifanya na hata sasa wanaandaa mkutano wao kahama.

    ReplyDelete
  6. ACT nao wamesema.

    ReplyDelete
  7. Hiyo chadema si uifute tu, kila siku wao, kupigwa wameshazoea, mahakamani wamezoea, KIFUTILIE MBALI

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad