Mwanamuziki wa Kenya Avril Apangua Tuhuma za Kutoka Kimapenzi na Diamond Platnumz

Msanii wa muziki kutoka nchini Kenya, Judith Mwangi 'Avril' ambaye alicheza kama video queen kwenye wimbo wa Diamond Platnumz 'Kesho' amefunguka na kusema hakuwahi kutoka kimapenzi na Diamond Platnumz kama ambavyo baadhi ya watu walivyokuwa wakidhani

Msanii Diamond Platnumz akiwa na msanii kutoka Kenya Avril.
huenda kuwa Diamond Platnumz baada ya video hiyo labda alitumia nafasi hiyo kutoka naye kimapenzi.

Avril kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio alisema kuwa yeye na Diamond Platnumz hawakufanya project nyingine yoyote zaidi ya kutengeneza video ile ya 'Kesho' japo alimuelezea Diamond kuwa ni msanii mpole sana na mwenye kupenda kazi yake na kujituma.

"Diamond ni rafiki yangu ni mtu poa sana, tumejuana kwa muda mfupi lakini ni msanii mwenye bidii ya kufanya kazi na kukutana na msanii mwenye bidii ni jambo zuri, hi mtu mzuri mpole hana maneno na watu. Najua vyombo vya habari vinampa sifa nyingi tofauti na yeye lakini ukikutana na yeye moja kwa moja ni mtu mzuri sana. Baada ya kufanya ile video ya kesho hakuna project nyingine tulifanya" alisema Avril

Mbali na hilo Avril alitaja wasani watano kutoka Tanzania ambao anawakubali na kuanza na Diamond Platnumz, Ommy Dimpoz, Raymond, Vanessa Mdee pamoja na Linah Sanga.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kina dada wengi wanakana sana kama wameshelala na diamond sijui kwanini. Kuna mdada mmarekani mondi alishatokaga nae enzi za wema unaambiwa mondi alikua akimposti picha zake mpaka kwenye bbm yake lakini yule dada mpaka leo hii anakataa amelala na mondi. Demu nasikia hataki hata kumuona na ummarufu aliokua nao Diamond

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad