Mzungu Aponzwa na Mkia wa Tembo

Tembo
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu Raia wa Afrika kusini Rudolf Van Niekerk miaka tano jela au faini ya Sh 65.8 milioni kwa kosa la kusafirisha nyara za serikali,

Akisoma mashtaka hayo Paul Kadushi, Wakili wa Serikali mbele  ya Huruma Shahidi Hakimu Mkazi katika mahakama hiyo amedai kuwa mtuhumiwa alikamatwa na nyara hizo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere   tarehe 17 Juni mwaka huu.

Kadushi amedai kuwa nyara hizo ni bangili iliyotengenezwa na mkia wa tembo yenye thamani ya Sh.32 milioni bila ya kibari.

Hata hivyo Niekerk Mtuhumiwa Raia wa Afrika Kusini  ambaye asili yake ni mzungu amekiri mashtaka hayo.

Shahidi, ambaye ni Hakimu aliyetoa hukumu hiyo awali amesikiliza upande wa mtetezi Gerrad Nangi, wakili wa mtuhumiwa ambapo amedai Mteja wake ni mgeni Tanzania na hajui sheria za nchi.
Aidha Nangi amedai mteja wake ni mgonjwa na anafamilia pia nimsaada mkubwa katika maendeleo ya Tanzania kwani yeye ni fundi mitambo katika kiwanda cha sukari cha kilombero.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad