Nchi 10 Zinazolipa Vizuri Mishahara Duniani...

Je, ulishawai kujiuliza nchi ambazo wafanyakazi wanalipwa mishahara ya juu? Hebu tuangalie nchi kumi ambazo wafanyakazi wanapata malipo makubwa ya kazi zao wanazofanya


#10 Ufaransa
Ufaransa ni nchi ya 7 yenye uchumi mkubwa zaidi duniani, Wafanyao kazi Ufaransa wanafanya kazi kwa mda mchache ni kama masaa 35 kwa wiki. Kwa wastani  kipato cha mfanyakazi wa Ufaransa ni $28,799 kwa mwaka baada ya kulipa kodi zote.


#9 Sweden
Kutokana na data za Bank kuu ya dunia,hii nchi nzuri ya kiscandinavia ni ya sita kwa uchumi wa ndani duniani. Sweden ni wazalishaji wakubwa wa mbao. Kwa wastani kipato chao ni $29,185 kwa mwaka baada ya makato yote ya kodi


#8 Canada
Canada majirani wa Marekani,ni nchi ya tatu yenye uhifadhi mkubwa wa mafuta duniani ikipitwa na
Venezuela na Saudi Arabia. Nchi hii pia ina utajiri mkubwa wa zinc, uranium, dhahabu na aluminium.
Kwa wastani kipato chao ni $29,356 kwa mwaka baada ya makato yote ya kodi


#7 Austria
Austria ni nchi ambayo ipo katikati ya Ulaya, Imeendelea sana kiviwanda na sekta ya utalii
inachangia asilimia 9 ya pato la ndani la taifa. Kwa wastani kipato chao ni $31,173 kwa mwaka baada ya makato yote ya kodi


#6 Germany
Germany ni nchi ya kwanza yenye uchumi mkubwa zaidi ulaya. Kwa wastani kipato chao ni $31,252 kwa mwaka baada ya makato yote ya kodi



#5 Australia
Australia ni moja kati ya nchi zenye uchumi imara zaidi duniani,ni wasafirishaji wakubwa wa madini na wanaagiza bidhaa chache sana kutoka nje.Katika swala la wastani wa utajiri, Australia ilishika nafasi ya pili duniani baada ya Switzerland mwaka 2013. Kwa wastani kipato chao ni $31,588 kwa mwaka baada ya makato yote ya kodi


#4 Switzerland
Uswisi inashika nafasi za juu katika utendaji bora wa serikali yao, ikiwa ni pamoja na uwazi wa serikali yao, uhuru wa raia, ubora wa maisha, ushindani wa kiuchumi na maendeleo ya binadamu. Kwa wastani kipato chao ni $33,491 kwa mwaka na wanafanya kazi masaa 35 tu kwa wiki.


#3 Norway
Norway ina utajiri mkubwa  wa maliasili ikiwa pamoja na mafuta,umeme wa maji,uvuvi na madini.Kwa wastani kipato chao ni $33,492 kwa mwaka


#2 Luxembourg
Luxembourg ni wasambazaji wakubwa wa chuma ulaya. Kwa wastani kipato chao ni $38,951 kwa mwaka


#1 USA
Pato la ndani kwa mwaka ni $55,000 na makato ya taxi ni asilimia 23.Wafanyakazi wa Marekani wanafanya kazi masaa 44 kwa wiki.
Tags

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Vitu vingine muwe mnafanya utafiti vizuri kabla ya kupotosha uma pato la wastani USA ni $16,000 tax free hiyo ya $44,000 umetoa wapi??? $44000 ni mshahara wa mtu wa kati na aliyekolifai si college leavers.
    Kwa mfano UK kipapo cha wastani/chini ni £16,000 subsidised at the rate of £7.20/hr on 40 hrs a week sasa huko USA rate yao kwa saa ni mbaya sana kwa mamilioni ya watu. EU yote masaa ni 35 by the law kasoro UK ambayo imejitoa.
    Chimbeni sana kabla ya kuweka humu kuepusha kuudanganya umma

    ReplyDelete
    Replies
    1. wewe unayesema haya unaishi USA? hata kwa kazi ya dukani ya chini ya kuuza au MC Donald wanalipwa kuanzai dola 10. Na bado wanataka kupandisha. Hizo dola 7 na 8 wanalipana hao wasio na vibali vya kazi acha uango wewe

      Delete
    2. Eti pato la wastani ni $16,00 USA? un kichaa wewe hapo juu? unajua maana ya wastani? manake ni average. Haiwezekani hata siku moja average salary ya USA ikawa ni 16,000. ukiniambia the lowest annual salary labda. yaani mtu wa chini analipwa average ya dola 16,000 kwa mwaka. Watu tunafanya kazi za kawaida na kwa mwaka tunapata zaidi ya dola 35,0000 we unasema nini wewe? tena hiyo ni kazi ya kufundisha chekechea ila uwe na degree. Msijifanye mnajua sisi tunaoishi huku ndio tunajua. USA wanalipa vizuri hata kazi za kijinga.

      Delete
    3. WEWE HAPO JUU NI MBULULAAAAZ KABISA. HAKUNA NAMNA PATO TA WASTANI LA USA LIKWA $16,000. UNACHEKESHA. THAT IS AVERAGE INCOME MY DEAR. TENA HUYO ALIYESEMA $44,000 AMEPUNGUZA. ACTUALLY THE AVERAGE NI 51,939. YAANI KAMA UNAJUA AVERAGE INAVYOCALCULETIWA. UNACHUKUA MISHAHARA YA WATU WOTE UNAJUMLISHA UNAPATA WASTANI. MSHAHARA WA CHINI KABISA LABDA MC DONALDS WANAOLIPA DOLA 8 KWA SAA UNAMPA MTU DOLA HIZO UNAZOSEMA WEWE ZA 16,000. MNAPENDAGA KUJIFANYA MNAJUA ILI TU MJIRIDHISHE. USA WATU WANALIPWA VIZURI UPENDE USIPENDE. SASA KUHUSU MATUMIZI HAYO NI AKILI YAKO LAKINI KULIPWA NI VIZURI SANA KULINGANISHA NA NCHI NYINGINE.

      Delete
    4. WEWE HAPO JUU NI MBULULAAAAZ KABISA. HAKUNA NAMNA PATO TA WASTANI LA USA LIKWA $16,000. UNACHEKESHA. THAT IS AVERAGE INCOME MY DEAR. TENA HUYO ALIYESEMA $44,000 AMEPUNGUZA. ACTUALLY THE AVERAGE NI 51,939. YAANI KAMA UNAJUA AVERAGE INAVYOCALCULETIWA. UNACHUKUA MISHAHARA YA WATU WOTE UNAJUMLISHA UNAPATA WASTANI. MSHAHARA WA CHINI KABISA LABDA MC DONALDS WANAOLIPA DOLA 8 KWA SAA UNAMPA MTU DOLA HIZO UNAZOSEMA WEWE ZA 16,000. MNAPENDAGA KUJIFANYA MNAJUA ILI TU MJIRIDHISHE. USA WATU WANALIPWA VIZURI UPENDE USIPENDE. SASA KUHUSU MATUMIZI HAYO NI AKILI YAKO LAKINI KULIPWA NI VIZURI SANA KULINGANISHA NA NCHI NYINGINE.

      Delete
  2. @anonymous 10;27 kabla ujapinga ulitakiwa ufanye uchuguzi sio kupinga wewe ndii unataka kupota umma ebu goggle median income in us hicho kilichowekwa hapo sio minimum wage wacha kujaribu kujifanya lematus

    ReplyDelete
  3. Huo utafiti wenu naona mmeutoa kijijini. Denmark inalipa vizuri mishahara kuliko Germany au Swaziland etc. Bomo

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad