NSSF Kuwaburuza Kortini Waajiri 10 Kwa Tuhuma za Kuchelewesha Michango ya Wafanyakazi

Waziri Jenista Mhagama amebariki mpango wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Iringa wa kutaka kuwafikisha waajiri 10 mahakamani kwa tuhuma za kuchelewesha michango ya wafanyakazi.

Waajiri hao kwa pamoja wanadaiwa kuisababishia NSSF hasara ya Sh497.17 milioni, ambazo ni malimbikizo ya michango waliyotakiwa kuiwasilisha.

Akizungumza katika ziara yake mkoani Iringa Alhamisi hii, Mhagama alisema uamuzi wa NSSF wa kutaka kuwafikisha mahakamani waajiri hao ni mzuri, unastahili kutekelezwa mapema.

Awali, Kaimu Meneja wa NSSF Mkoa wa Iringa, Patrick Gandye alisema ofisi yake imeamua kuwafikisha mahakamani waajiri kumi kutokana na kitendo chao cha kutowasilisha michango ya wafanyakazi, jambo linalokwamisha utekelezaji wa majukumu yake.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad