Pamoja ya Yote Lakini Kuna Kubwa la Kujifunza Toka CCM

Kwanza niseme tu kuwa mimi naunga mkono upinzani, lakini nimeona kuandika uzi huu baada ya kuona kuna kitu ambacho sisi wapinzani tunachakujifunza toka kwa CCM. Pamoja na mapungufu mengi ya chama tawala lakini bado angalau wana mifumo ya kidemocrasia hata kama haijakamilika lakini kitendo cha kubadirisha viongozi wakuu kwenye chama ni kitu cha kuigwa. Hivi ndani ya vyama vyetu hakuna watu wengine wanaoweza kuongoza?? Kwamba lazima wawe ni wale wale tu. Lini Mbowe atapumzika, Lini Maalim Seif atapumzika, lini Mbatia atapumzika du, na isingekuwa mvutano pengine na Lipumba angekuwemo mpaka leo. Tunahitaji fikra mpya ndani ya vyama vya upinzani kama ni kweli tunahubiri democrasia. Inawezekana nikawa kinyume na wengi lakini, nimeona niwe muwazi kutoa maoni yangu.

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hata UKAWA wakishika dola uongozi wa juu utabadulika
    Kulingana na katiba

    Viongozi wa ukawa huchaguliwa
    Acheni ushamba ccm

    ReplyDelete
    Replies
    1. yaani wewe ndo zumbukuku chadema wana demokrasia gani ya mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti na kuzuia wengine kushika nafasi ya uwenyekiti?????

      Delete
  2. Demokrasia halisi kiongozi akishndwa uchaguzi anafunga virago unless viongozi wa chama hicho ni madikteta au hakuna wenye upeo zaidi ya walioko madarakani.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acha umbea wewe kati ya Chadema na ccm nani asiye na upeo!! rejea mazungumzo ya mwenyekiti wenu mstaafu (kuwa ccm sasa inahitaji wasomi kujiunga na chama hicho) kwa maana hiyo ni kwamba huko upeo wao ni majungu ndiyo mtaji wa kujiunga na chama kama ulivyo wewe.

      Delete
    2. Ila nilicho jifunza kwa kuwaangalia na kuwasikiliza hawa jamaa wa ccm ni kwamba matumbo yao yapo joto kwa kumuofia Maghufuli mwe!!

      Delete
  3. Duuh,hili nalo neno!

    ReplyDelete
  4. Ukionesha dalili za kutaka uenyekiti Chadema unatimuliwa kama sio kuuwawa kabisa, muulize Zito Kabwe! CCM ndio 'BABA LAO' bingwa wa demokrasia......nani anabisha?????

    ReplyDelete
  5. Upinzani ni kama Private Company huwezi kuachia ngazi ktk kampuni uliyoianzisha mwenyewe labda umfanye mwanao au mkeo kushika madaraka si waajiriwa wengine.
    CHADEMA ni ya WATU na CUF pia ni ya WATU

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad